Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu
Nchemba(katikati), akizungumza na watendaji wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kupambana na Dawa za Kulevya na Uhalifu(UNODC), Bi. Kaitlin Meredi (kulia) na Johan Kruger(kushoto), walipomtembelea
ofisini kwake,jijini Dar es Salaam,leo. Ziara hiyo ikiwa na lengo la kujadili
njia muafaka za kukabiliana na biashara, matumizi na athari za dawa za kulevya
kwa jamii.
Mkuu wa Kitengo cha Kupambana na
Biashara Haramu ya Dawa za Kulevya
kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la Kupambana na Dawa za Kulevya na
Uhalifu(UNODC),Johan Kruger(kushoto), akizungumza na Waziri wa Mambo ya Ndani
ya Nchi, Mwigulu Nchemba (katikati),walipomtembelea ofisini kwake kwa ajili ya
kuzungumzia juhudi mbalimbali za kupambana
na biashara haramu ya Dawa za Kulevya.Kulia ni Mratibu wa Kupambana na Uhalifu wa Majini, Kaitlin
Meredith.
Mratibu
wa Programu ya Kupambana na
Uhalifu wa Majini kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la Kupambana na Dawa za
Kulevya na Uhalifu(UNODC), Kaitlin Meredith (kulia), akizungumza na Waziri wa
Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba, masuala yanayohusu udhibiti wa uhalifu unaofanyika majini
walipomtembelea ofisini kwake, jijini Dar es Salaam, leo.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,
Mwigulu Nchemba (katikati),akiagana na Mratibu
wa Programu ya Kupambana na
Uhalifu wa Majini, Kaitlin Meredith, mara baada ya kumaliza mazungumzo yaliyofanyika
ofisini kwa waziri, jijini Dar es Salaam,
leo.Kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Kupambana na Biashara Haramu ya Dawa za Kulevya kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la
Kupambana na Dawa za Kulevya na Uhalifu(UNODC), Johan Kruger (Picha Zote na
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi)
IMEANDALIWA NA KITENGO CHA MAWASILIANO
SERIKALINI-WIZARA YA MAMBO YA MAMBO YA NDANI YA NCHI)
No comments:
Post a Comment