Kutoka
Kushoto ni Eng Sadick Chakka Mhandisi
wa Maji Wilaya ya Ikungi, Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Miraji jumanne Mtaturu, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya
Wilaya ya Ikungi Rustika Turuka,
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi Ally J. Mwanga, na Kulia ni Abel Suri Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya
Ikungi
Na Mathias
Canal, Singida
Jeshi la polisi Wilaya ya Ikungi Mkoani Singida limemtia
nguvuni Diwani wa Kata ya Iseke kwa tiketi ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo
CHADEMA Emmanuely Njingu kwa kosa la
kukwamisha shughuli za serikali kwa kuzuia watendaji wa serikali kufanya kazi
yao ikiwemo ukusanyaji wa mapato.
Njingu ambaye alikuwa mjumbe wa kamati ya fedha awali kabla
ya kuwekwa nguvuni na jeshi la polisi alivuliwa ujumbe wa kamati hiyo kutokana
na kukiuka taratibu na makubaliano ya baraza la madiwani jambo ambalo
limepelekea kuhamishiwa katikakamati nyingine.
Akitoa taarifa ya kukamatwa kwa diwani huyo Mwenyekiti wa
Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi ambaye ni Diwani wa Kata ya Irisia Ally Juma Mwanga amesema kuwa Diwani
huyo amekamatwa kwa mujibu wa sheria hivyo yeye kama mwenyekiti hawezi
kuingilia taratibu, sheria,na kanuni za serikali.
Mwanga
amesema kuwa tarehe 19 mwezi Julai moja ya maadhimio ya kamati ya fedha na
vikao vya baraza ilikuwa ni kuimarisha ukusanyaji wa mapato ya Halmashauri
lakini diwani huyo amekiuka makubaliano hayo kwa kung’oa mageti ya vizuizi vya
barabarani kwa ajili ya ukaguzi wa mazao jambo ambalo limepelekea kuzorota kwa ukusanyaji
wa mapato ya Halmashauri.
Ameongeza kuwa Mjumbe yeyote anayekiuka maazimio
wanayokubaliana na kutoa siri za kamati adhabu yake kisheriani kupoteza sifa ya
kuwa mjumbe wa kamati husika.
Amesema diwani huyo ameondoshwa katika nafasi hiyo baada ya maridhiano
ya kamati hiyo na kukubaliana kumuhamishia katika kamati nyingine ya huduma za
uchumi.
“Jambo mkishakubaliana kisheria tena kwenye vikao vya
kisheria maana yake linakuwa ni sheria hivyo kwa kiongozi yeyote akikiuka
taratibu za kisheria zinachukua mkondo wake, kanuni za Halmashauri ni za watu
wote hazichagui upande mmoja” Alisema
Mwanga
Hapo jana Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Miraji Jumanne Mtaturu alihutubia Baraza la madiwani wa Halmashauri
ya Wilaya hiyo ikiwa ni mara yake ya mwanzo kabisa tangu alipochaguliwa na Rais
John Magufuli kuwa Mkuu wa Wilaya
hiyo ambapo pamoja na kuzungumzia kuwepo kwa changemoto ya uhaba wa maabara, afya
duni na miundombinu pia alizungumzia kuhusu ukusanyaji hafifu wa mapato jambo
ambalo linairudisha nyuma Halmashauri ya Wilaya hiyo.
Bajeti ya Wilaya ya Ikungi kwa Mwaka 2013/2014 ilikuwa na
Shilingi 509,701,044 namakusanyoyakeyakawa ni 338,325,000 ambapo hata hivyo
mwaka ulimalizika kwa kuwa na upungufuwa shilingi 171,376,044.
Mwaka 2014/2015 ilipangwa bajeti ya shilingi 631,455,000 lakini
makusanyo yake yakawa ni shilingi 457,555,172 ambapo mwaka ulimalizika kwa
kukusanya 173,899,828.
Mwaka wa bajeti 2015/2016 bajeti ya Halmashauri iliyopangwa
ilikuwa ni shilingi 1,127,030,000 makusanyo yalikuwa ni 679,283,000 ambapo hata
hivyo mwaka ulimalizika kwa kwa kuwa na upungufu wa shilingi 450,747,000 hivyo
kwa miaka mitatu Halmashauri hiyo imeshindwa kufikia malengo ya ukusanyaji.
Mwanga amesema kuwa Kutofikiwa malengo hayo kumesababishwa
na kutopewa ushirikiano watendaji katika ukusanyaji wa mapato hii ikiwa ni
kufuatia kauli za mazuio zinazotolewa na baadhi ya wanasiasa.
Hata hivyo ametoa Mwito kwa viongozi wa serikali, wanasiasa,
taasisi za dini na wananchi kushirikiana kwa pamoja ili kufikia malengo ya
kuifanya Ikungi kukua kiuchumi .
No comments:
Post a Comment