Kutoka Kushoto ni Eng
Sadick Chakka Mhandisi wa Maji Wilaya ya Ikungi, Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Miraji Jumanne Mtaturu, Mkurugenzi
Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi Rustika Turuka, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi Ally J. Mwanga, na Kulia ni Abel Suri Makamu Mwenyekiti wa
Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi wakisikiliza kwa makini hoja za madiwani wakati wa kikao cha Baraza la madiwani wa Wilaya hiyo.
Aliyesimama ni Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Miraji Jumanne Mtaturu akisisitiza
jambo
Umakini umeonekana wazi wakati wa uwasilishwaji wa
hotuba ya Mkuu wa Wilaya ya ikungi Miraji
Jumanne Mtaturu
Mwenyekiti wa kamati ya huduma za jamii ambaye ni Diwani
wa Kata ya Issuna Steven Misai akitoa
neno la shukrani kwa hotuba ya mkuu wa Wilaya ya ikungi
Na
Mathias Canal, Singida
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Miraji Jumanne Mtaturu amewaonya baadhi ya wanasiasa hususani
madiwani katika Wilaya hiyo kupitia matamko yao ya kuzuia ukusanyaji wa ushuru
au kupiga vita vizuizi vilivyowekwa katika kata zote.
Madiwani hao wanatumia vibaya Uelewa mdogo wa
wananchi kwa kuwazuia kuchangia shughuli za maendeleo na ulipaji kodi hivyo
amewaagiza madiwani wote kuacha kuwatumia wananchi kwa muktadha wa kuwanyima
ufahamu bali wawe mstari wa mbele kuwaelimisha kwa kushirikiana na wataalamu
wanaopita kukusanya kodi katika maeneo yao.
Dc
Mtaturu ameyasema hayo wakati wa kikao chake cha kwanza cha
Baraza la madiwani la Wilaya hiyo tangu alipoteuliwa na Rais John Magufuli kushiriki kwenye baraza la madiwani ambapo
pamoja na hotuba yake hiyo amewapongeza madiwani wote kwa kuaminiwa na
kuchaguliwa kwa ajili ya kuwawakilisha wananchi katika kata zao.
Dc Mtaturu amesema
kuwa Baraza la madiwani ndio injini
kuu ya maendeleo ya Wilaya, hivyo kama kukiwa na Baraza lisilotimiza wajibu
wake kamwe Wilaya haiwezi kutoka kwenye kadhia iliyopo hususani katika sekta ya
Kilimo, Mifugo, uvuvi, elimu, afya na miundombinu.
“Wilaya yetu bado ina
changamoto nyingi sana, Natambua Wananchi wengi bado ni masikini kama sio wenye
kipato cha chini sana, Natambua Wananchi wengi wanajishughulisha na Kilimo na
Ufugaji ingawa wapo Wachimbaji wadogo wa Madini na Wafanyabiashara pia lakini natambua
huduma za jamii pamoja na miundombinu ni changamoto kubwa sana”
“Tumekuwa Wilaya ya
kuomba chakula cha msaada kila mwaka, maambukizi ya Virusi vya Ukimwi VVU
yanazidi kupanda, Elimu inazidi kushuka, mapato ya Halmashauri yameshuka,
wananchi wetu wamekuwa wakifuga na kulima kilimo kile kile cha mazoea, huduma
ya maji safi na salama imeendelea kuwa changamoto kwetu, Vituo vya Afya na Zahanati
havitoshelezi mahitaji” Alisema Mtaturu
Kwenye
Huduma ya Afya katika Vijiji 101 vilivyopo Wilayani Ikungi kuna Zahanati 34,
Vituo vya Afya 3 na Hospitali 2, kwa uwiano huu zisipofanyika jitihada zaidi hali
ya wananchi itakuwa mbaya zaidi.
Hivyo
Mkuu huyo wa Wilaya hiyo alisema kuwa Madiwani wote wanatakiwa kuwa na mpango
mkakati wa kuhakikisha huduma za Afya zinapatikana kirahisi.
Katika
hotuba yake Dc Mtaturu ameeleza kuwa
Ni lazima kwenye Kamati za Maendeleo za Kata (WDC) kuanzishwe mipango ya
kuhakikisha kunapunguzwa Vifo vya Wakinamama Wajawazito na Watoto kwa kuweka
mikakati itakayohakikisha Wananchi wote hawaendi umbali mrefu kutafuta huduma
za Afya.
“Katika suala hili
la Afya ningependa kuzungumzia mabadiliko katika Sekta ya Afya yanayoendelea
hapa Nchini katika utoaji wa huduma. Mabadiliko
haya yana lengo la kuinua kiwango cha ubora wa huduma za afya zinazotolewa kwa
wananchi na kuongeza kiwango cha uwajibikaji kwa wasimamizi na watoaji wa
huduma hizo. Ili kufanikisha lengo hilo,
madaraka, majukumu na kazi, rasilimali zaidi za afya zinahitajika kwa kuitaka
jamii kuchangia katika mifuko ya Afya ya Jamii (CHF)” Alisema Mtaturu
Katika Mfuko wa
Afya (CHF) Kaya moja itatakiwa kuchangia Tsh. 10,000/= na atatibiwa
Baba, Mama na Watoto wanne kwa mwaka mzima, hivyo Mwananchi akiuza kuku mmoja
tu anatosha kumtibia yeye mwenyewe na familia yake kwa mwaka mzima.
Mwananchi
asipojiunga na huduma hii atatakiwa kutoa Papo kwa Papo Tsh. 7,000/= pale anapougua hii elfu
saba ni ya kumuona Daktari bila dawa, Mwananchi huyu akiuguliwa na watu watano,
itamlazimu kutoa Tsh. 35,000/= kwa hiyo Mwananchi ambaye hajajiunga na CHF
atapata hasara ya Tsh. 25,000/= na wakati mwingine anaweza akauguliwa akiwa hana hata hela ya kutibiana hatimaye anahatarisha
maisha ya watu wake wa karibu.
Dc Mtaturu
amewataka Viongozi hao kujitafakari kwa nini waliomba ridhaa ya kuwaongoza
Wananchi wa Ikungi, kama waliomba nafasi hiyo kwa ajili ya kuwatumikia Wananchi
lakini kwenye Kata zao Shule za Sekondari hazina Maabara, hakuna Zahanati na
Kituo cha Afya, hakuna barabara, hakuna huduma ya maji safi na salama na hakuna
Shule; Wanafunzi wanatembea umbali mrefu kufuata Shule na hawana mpango wowote
ule wa kusogeza karibu huduma hizi basi wanatakiwa kujitafakari upya.
Mkuu
huyo wa Wilaya ameahidi kushirikiana na kila Kiongozi bila kujali itikadi ya
Chama chake, Dini yake au rangi yake katika kuwaletea maendeleo Wananchi wa
Ikungi.
Akitoa
salamu za shukrani kwa niaba ya Madiwani wote kwa hotuba ya Mkuu wa Wilaya ya
Ikungi, Mwenyekiti wa kamati ya huduma za jamii ambaye ni Diwani wa Kata ya
Issuna Steven Misai amesema kuwa Hotuba ya Mkuu huyo inaonyesha taswira
mpya ya kuinusuru Wilaya hiyo katika sekta ya elimu, afya, na miundombinu.
Missai
alisema kuwa maagizo ya hotuba yake yatafanyiwa kazi na madiwani wote ili
kuifanya wilaya ya Ikungi kuwa nguzo katika sekta hizo hususani ujenzi wa maabara.
No comments:
Post a Comment