Mwenyekiti wa kamati ya
ulinzi na usalama wa Wilaya ya ikungi ambaye ni Mkuu wa Wilaya Miraji Jumanne
Mtaturu akikagua vijana wa mafunzo ya Mgambo kutoka vijiji vitano vya
Dung’unyi, Munkinya, Kipumbuiko, Samaka na Damankiya vinavyounda Kata ya Dung’unyi
katika Tarafa ya Ikungi.
Kundi la vijana wa Mgambo kutoka
Kijiji cha Ighombwe, Jerumani, na Mahonda wakionyesha umahiri wao katika
mafunzo waliyoyapata mbele ya mgeni rasmi kwenye ufunguzi wa mafunzo hayo
katika Tarafa ya Sepuka.
Mwenyekiti wa kamati ya
ulinzi na usalama wa Wilaya ya ikungi ambaye ni Mkuu wa Wilaya Miraji Jumanne
Mtaturu akiwa kwenye picha ya pamoja na wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama
ya Wilaya ya Ikungi.
Kundi la vijana wa Mgambo
kutoka Kijiji cha Ighombwe, Jerumani, na Mahonda wakimsikiliza mgeni rasmi
kwenye ufunguzi wa mafunzo hayo katika Tarafa ya Sepuka.
Mwenyekiti wa kamati ya
ulinzi na usalama wa Wilaya ya ikungi ambaye ni Mkuu wa Wilaya Miraji Jumanne
Mtaturu akijadili jambo na Mshauri wa Mgambo Wilaya ya Ikungi Fortunatus
Ndalama.
Mkuu wa Wilaya Miraji Jumanne
Mtaturu akizungumza na watendaji Kata, na viongozi wa vijiji mara baada ya
ufunguzi wa mafunzo ya mgambo yatakayodumu kwa wiki 16.
Na Mathias Canal, Singida
Wiki 16, Miezi minne
itatosha kuwakutanisha pamoja vijana wa kata mbalimbali Wilayani Ikungi kwa
pamoja wakipatiwa mafunzo ya Mgambo hususani kujifunza uzalendo, Mbinu za
medani za kupambana na uhalifu, Kuimarisha nidhamu na kujituma.
Hayo yamebainishwa na
Mwenyekiti wa kamati ya Ulinzi na Usalama ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Ikungi
Miraji Jumanne Mtaturu wakati akifungua rasmi mafunzo hayo yatakayojikita pia
katika kuimarisha utu na uadilifu.
Mtaturu amesema kuwa
vijana wote walioamua kujitolea katika mafunzo hayo kwa ridhaa yao watapaswa
kuwekwa katika kumbukumbu ya vijana ambao baada ya kumaliza mafunzo
wataanzishiwa vikundi vya ujasiriamali ambavyo vitasimamiwa na Ofisi ya Mkuu wa
Wilaya.
"Tanzania ina wimbi
la vijana wengi ambao wanajiamulia maisha wenyewe kutokana na wazazi wao
kuyakimbia majukumu yao ya kuwalea watoto wao katika maadili mema ya kumjua
Mungu na nidhamu kwa kila mtu kwenye jamii hivyo sisi kama serikali ngazi ya
Wilaya tutahakikisha Vijana hawa wanaimarika katika maadili mema" Alisema
Mtaturu
Dc Mtaturu amesema kuwa mara baada ya kumalizika kwa
mafunzo hayo vijana hao watapaswa kuamua wanataka kujishughulisha na nini kati
ya ufugaji na kilimo cha kisasa ambapo ofisi ya mkuu wa Wilaya itasimamia
kuhakikisha wanafanikiwa katika malengo yao.
Sambamba na hayo
amewaeleza vijana hao kuwa serikali ina mamlaka ya kuwasaidia watanzania
kujikwamua katika wimbi kubwa la umasikini lakini pia vijana na watanzania kwa
ujumla wanapaswa kutumia muda wao mwingi kujishughulisha na shughuli za
uzalishaji mali kwa kufanya kazi sio kucheza bao, kujihusisha na vikundi ovu,
kunywa pombe, Ngono zembe ama kucheza Pool Table wakati wa kazi.
Dc Mtaturu amewapongeza vijana hao kwa kujitolea kwa
moyo mmoja kushiriki katika mafunzo hayo ambapo amesema kuwa mafunzo
wanayoyapata sio mateso ila ni sehemu ya kuwaimarisha kimwili na kiakili,
Kujifunza maadili mema, ili kuwa na uchungu na nchi yetu.
Mafunzo ya mgambo
yaliyofunguliwa na Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Miraji Jumanne Mtaturu yanahusisha Tarafa mbili ya Ikungi na Sepuka
ambapo katika Tarafa ya Ikungi vijana wa kiume waliojitokeza ni 138 huku
wanawake wakiwa 6.
Kwa upande wa Tarafa ya
Sepuka kuna jumla ya vijana 210 ambapo vijana wa kiume ni 206 na wanawake ni wa
4.
Katika ufunguzi wa
Mafunzo hayo katika Tarafa hizo mbili Mkuu huyo wa Wilaya ya Ikungi aliambatana
na Wajumbe wa kamati ya Ulinzi na usalama ya Wilaya.
Dc Mtaturu amesisitiza kuwa mgambo wanajulikana kama
jeshi la akiba ambapo wajibu wao Mkubwa ni kushirikiana na jeshi la polisi na
Jamii katika kuimarisha ulinzi wa watu na Mali zao.
No comments:
Post a Comment