Naibu Inspekta Jenerali wa Polisi, Abdulrahman Kaniki |
NA FRANK GEOFRAY-JESHI LA POLISI, DODOMA
JESHI
la Polisi nchini litaendelea kuboresha vituo vyake vya afya ili
kuwawezesha Askari kupata huduma zilizo bora jambo ambalo litawawezesha
kufanya kazi wakiwa na afya pamoja na morali katika kupambana na uhalifu
nchini.
Hayo
yamesemwa na Naibu Inspekta Jenerali wa Polisi, Abdulrahman Kaniki
Mkoani Dodoma wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa kutathmini mradi wa
kupambana na ukimwi na kifua kikuu unaotekelezwa na Jeshi la Polisi
katika vituo vyake vya Afya kumi na tano hapa nchini kwa ufadhili wa
shirika lisilo la kiserikali la JSI-AIDS Free tawi la Tanzania.
Kaniki
alizitaja juhudi zinazoendelea kuchukuliwa kuwa ni pamoja na kuboresha
majengo, kutoa mafunzo kwa watendaji pamoja na kuhakikisha kuwa
hospitali za Polisi zinakuwa na vifaa bora kwa mujibu wa viwango
vilivyowekwa na Wizara ya Afya .
Aidha
alitoa wito kwa Shirika la JSI-AIDS Free kuongeza wigo wa huduma zake
katika vituo vngine ambavyo havijafikiwa na mradi huo hapa nchini ili
kuhakikisha kuwa kila mahali palipo na kituo cha Afya cha Polisi
kunakuwepo na mradi huo ambao umesaidia sana askari na watumiaji wengine
wa huduma hizo.
Kwa
upande wake Mwakilishi mkazi wa Shirika hilo kwa upande wa Tanzania
Dk.Beati Mboya alisema lengo la mkutano huo ni kufanya tathmini ili
kubaini mafanikio na changamoto zinazovikabili vituo vinavyotekeleza
mradi huo ilikuzipatia ufumbuzi.
Alisema
wanatarajia kufanya tathmini hiyo kila baada ya miezi mitatu ili
kuhakikisha hakuna ucheleweshaji katika kutoa huduma baada ya kubaini
changamoto na kuzifanyia kazi kwa haraka.
Naye
Kamanda wa Kikosi cha Afya cha Jeshi la Polisi, Kamishna Msaidizi
Mwandamizi wa Polisi SACP Paul Kasabago alisema kikosi hicho kitaendelea
kutoa huduma zilizobora ili kuimarisha afya za Askari na familia zao
kote nchini licha ya kukabiliwa na upungufu wa wahudumu wa Afya.
No comments:
Post a Comment