NA K-VIS MEDIA NA MASHIRIKA YA HABARI
Shughuli
ZOTE KWENYE UWANJA WA NDEGE WA Kimataifa wa Dubai, Himarati, zimesimama
baada ya ndege iliyobeba abiria 300, kupata hitilafu ilipotua na kasha
kuwaka moto.
Ndege hiyo Emirates Boeng 777 ilikuwa ikisafiri kutoka Thiruvananthapuram
nchini India wakati ilipokumbwa na mkasa huo mapema leo Agosti 3, 2016.
Kwa
mujibu wa taarifa za vyombo vya habari, abiria wote 282 na wahudumu wa
ndege 18 wa ndege hiyo chapa EK521 waliokolewa na wako salama ukiachilia
mbali mishtuko kutokanana dhahma hiyo.
Mamlaka za Dubai hazijatoa maelezo zaidi kuhusiana na ajali hiyo.
No comments:
Post a Comment