Naibu
Waziri wa Habari Utamaduni sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura
akikabidhi bendera kwa timu ya Tanzania inayoenda kushiriki katika
mashindano ya Olimpiki kwa mwaka 2016 nchini Brazil Agosti 1, 2016.
Mkurugenzi
Mkuu wa Multichoice Tanzania Bw. Maharage Chande akishukuru Serikali
kwa fursa ya kuunga mkono jitihada za kuendeleza michezo wakati wa hafla
ya kuwaaga wanamichezo wanaokwenda kuiwakilisha Tanzania nchini Brazil
katika mashindano ya Olimpiki kwa mwaka 2016 nchini Brazil Agosti 1,
2016.
Mkuu
wa Kitengo cha Mawasiliano TTB Bw. Godfrey Tengeneza akitoa nasaha
zake kwa wawakilishi wa Tanzania katika mashindano ya Olimpiki kwenda
kutangaza utalii wa Tanzania wakati wa hafla ya kuwaaga wanamichezo
wanaokwenda kuiwakilisha Tanzania nchini Brazil katika mashindano ya
Olimpiki kwa mwaka 2016 nchini Brazil Agosti 1, 2016.
Zikiwa
zimebaki siku chache kabla kuanza rasmi michezo ya 31 ya Olimpiki mjini
Rio de Janeiro nchini Brazil inayotarajiwa kuanza Ijumaa ya Agosti 4,
2016 katika mji wa Sao Paulo na Rio De Jeneiro nchini Brazil wawakilishi
wa Tanzania katika michuano hiyo wamepata baraka zote kutoka kwa
Serikali na kukabidhiwa bendera ya Taifa kabla ya kwenda kuipeperusha
nchini Brazil.
Akikabidhi
bendera kwa timu hiyo Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na
Michezo Mhe. Annastazia Wambura aliwataka washiriki wanaokwenda
kuiwakilisha nchi kwenye mashindano ya Olimpiki mwaka huu huko Rio De
Jeneiro nchini Brazil kujituma na kuhakikisha wanafanya vizuri ili
warudi na medali.
Mhe.
Annastazia Wambura alisema kuwa wanapokwenda kuiwakilisha waamini kuwa
macho na masikio ya watanzania wote yapo kwao kwahiyo wajitahidi kadri
ya uwezo wao kuweza kuhakikisha watakapokuwa wanarejea basi waje wakiwa
wamevaa medali zao.
”
Mnakwenda katika mashindano ya Olimpiki macho yote ya watanzania yapo
kwenu tunategemea mkiwa mnarudi basi tutakuja kuwapokea mkiwa na medali
zenu kifuani na hilo linawezekana kama mtajituma mkiwa na ari ya
ushindi”.
Aidha
Katibu Mkuu wa Kamati ya Olimpiki Tanzania , Filbert Bayi alisema kuwa
kwa mwaka huu washiriki wamekaa kambi katika sehemu tofauti nchini na
wengine wakiwa nje ya nchi na hilo limefanikisha kuweza kujifua vyema na
kujiandaa ili kuweza kurejesha ushindi nyumbani.
Akizungumzia
mara baada ya kukabidhiwa bendera Kocha wa timu ya kuogelea Bw.
Alexandra Mwaipasi alisema kuwa wachezaji wake wameiva kwani mwanzoni
walikuwa na changamoto ya kupata mabwawa yenye viwango vinavyoendana na
mashindano hayo ili kwa matayarisho aliyowapatia wachezaji wake
anahakika watarudi na medali.
Moja
ya washiriki wa mchezo wa kuogelea katika mashindano ya Olimpiki kwa
mwaka 2016 Magdalena Mosha alisema kuwa amejiandaa vizuri na anaamini
kwa miaka aliyoshiriki kwenye mashindano ya Olimpiki ya Beijing na
London yamempa uelewa zaidi wa nini anatakiwa kufanya na kuyafanyia kazi
mazoezi aliyoyapata nchini Australia ili kurudi na ushindi.
Naye
mmoja wa wawakilishi katika mchezo wa Judo, Adrew Thomas alisema
amejiandaa vizuri kwa ajili ya mashindano hayo na yuko tayari
kuiwakilisha Tanzania na kuleta ushindi na pia kuitangaza Tanzania
katika michezo na utalii uliopo kwa kuvitangaza vivutio vilivyopo
nchini.
Kwa
upande wake Sara Ramadhani ambaye ni mwakilishi mwanamke pekee katika
mshindano hayo kwa wakimbiaji wa Marathon alisema yuko vizuri
kuipeperusha bendera ya taifa na kuitangaza Tanzania kimataifa kwa
kushindana na kushinda medali hivyo kuiletea sifa nchini.
Mmoja
wa wadhamini wa safari hiyo kampuni ya Multichoice Africa, imewataka
washiriki hao kujituma zaidi kwani watanzania wote watakuwa
wanawaangalia kupitia chaneli zao zinazopatikana kwenye kisimbuzi cha
DSTV.
Katika
mchango wao kwa wawakilishi hao Kampuni ya ving’amuzi ya Dstv imetoa
mchango wa kuwakutanisha pamoja kwa kuandaa hafla ya kuwaaga wawakilishi
hao ikiwa ni moja ya kuwatia moyo waende kupambana na kushinda katika
michezo mbalimbali na kuliletea sifa taifa.
Akizungumza
kwa niaba ya kampuni hiyo Mkurugenzi wa Multichoice Tanzania Maharage
Chande alisema mwaka huu mashindano yote yatakuwa yakioneshwa moja kwa
moja kupitia channeli za Super Sport na itawapa fursa watanzania
kuwashuhudia wawakilishi wao kwenye mashindano hayo makubwa duniani.
Bodi
ya Utalii nayo haikuwa nyuma kuwapa nguvu na morali wawakilishi wa
Tanzania katika mashindano ya Olimpiki kwenda kufanya vizuri katika
mashindano hayo na pia kutangaza vivutio vilivyopo nchini kwa mataifa
mbalimbali yanayoshiriki mashindano hayo kwa kuwapatia vifurushi kwa
ajili ya kusambaza ujumbe kuhusu utalii wa Tanzania.
Akitoa
nasaha zake kwa wawakilishi hao Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano TTB
Bw. Godfrey Tengeneza aliwaasa wawakilishi hao kujituma kwa bidii na
kutangaza nchi kupitia michezo na pia watumie fursa hiyo kutangaza
vivutio vilivyopo Tanzania kwa kueneza habari kuhusu utalii Tanzania.
“Mtakapokuwa
huko mbali na kushiriki katika michezo muitangaze nchi yetu kwa vivutio
vilivyopo nchini ili tuzidi kupata watalii wengi kutoka duniani kote”.
Timu
ya Tanzania inayoenda kushiriki mashindano ya 31 ya Olimpiki nchini
Brazil inawakilishwa na wachezaji saba ambao ni waogeleaji wawili
Magdalena Mosha anayeenda kwa mara ya tatu kwa upande wa wanawake huku
Hilal Hilal akienda kwa mara ya kwanza kwa upande wa wanaume na wote
watakuwa ni waogeleaji kwa umbali wa mita 50.
Wengine
ni Fabian Joseph, Said Juma Makula na Alphonce Felix Simbu
watakaokimbia marathon kwa wanaume na Sara Ramadhani ambaye ni mwanamke
pekee anayeiwakilisha Tanzania katika mbio za marathon.
Na kwa upande wa mchezo wa Judo Tanzania itawakilishwa na Adrew Thomas Mulugu katika uzito wa kilogramu 73.
Katika
mashindano ya Olimpiki mwaka huu takribani M yanatarajiwa kushindana
katika michezo mbalimbali huku Marekani ikiongoza kuwa na wachezaji
wengi zaidi katika mashindano hayo ikiwa na wachezaji 550 ikifuatiwa na
Brazil iliyo na wachezaji 450 na China inayowakilishwa na wachezaji 380.
No comments:
Post a Comment