Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Saturday 6 September 2014

MIMBA ZAWAKIMBIZA WANAFUNZI 66 DARASANI!


Na Amini Yassin, Mwananchi

Rufiji. Wanafunzi 66 wa kike katika shule 17 za sekondari ikiwemo Sekondari ya Wama Nakayama iliyopo Nyamisati, Kata ya Salale wilayani hapa inayomilikiwa na mke wa Rais, Mama Salma Kikwete wameacha masomo baada ya kupewa ujauzito.
Takwimu hizo ambazo ni kati ya mwaka 2012 hadi 2014 zimetolewa na Ofisa Elimu Sekondari Adnan Mwenda katika Kongomano la Wadau wa Elimu lililofanyika Kibiti, ambapo pamoja na mambo mengine lilijadili changamoto mbalimbali za elimu na namna ya kukabiliana nazo .
Alisema kwa mwaka 2012 wasichana 17 kutoka shule tano za sekondari, walipewa ujauzito, huku mwaka 2013 wakiwa wasichana 28 kutoka shule 12, ikiwemo ya Wama Nakayama.
“Mwaka 2014 wanafunzi 21 kutoka shule nane za sekondari walipewa ujauzito na kuacha masomo,” alisema Mwenda.
Alizitaja shule hizo na idadi ya walipata mimba kuwa ni Ikwiriri (10), Kazamoyo (8), Ngorongo (2), Zimbwini (9), Kikale (3), Msafiri (3), Mchukwi (3), Mahege (4), Mkongo (3), Ngorongo (1), Nyamisati (5).
Nyingine ni Ruaruke (1), Mwaseni (3), Utete (1), Mtanga delta (1), Mjawa (2), Mohoro (3) na Wama Nakayama (3).
Alisema kuwa sababu zinazochangia wasichana hao kupata ujauzito ni wazazi kushindwa kuwapa huduma zinazostahili hivyo kujiingiza katika vitendo vya ngono ili kupata mahitaji muhimu wanayohitaji.
Mwenda alidai kuwa sababu nyingine ni wanafunzi kubadilisha mazingira tofauti na yale waliyoyazoea ambapo vishawishi ni vingi kuliko katika mazingira waliyoyazoea. Kuhusu changamoto za uendeshaji wa elimu ya sekondari Rufiji, Mwenda alitaja upungufu wa walimu wa sayansi, uchache wa wanafunzi kuanzia kidato cha kwanza hadi cha nne.
Wakiachangia kongamano hilo Shabani Matwebe na Abdalah Mselemo walisema kuwa wazazi ndiyo chanzo cha watoto wa kike kupata ujauzito kutokana na watoto hao kukosa mahitaji muhimu kwao wawapo shuleni.
Walisema kuwa wanaowatia mimba wanafunzi wamekuwa hawachukuliwi hatua za kisheria hali inayochochea vitendo hivyo kuongezeka.
CREDIT: MWANANCHI

No comments:

Post a Comment