Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Saturday 27 September 2014

AJALI 10,586 ZATOKEA MWAKA HUU, BODABODA ZAUA WATU 608!


Na Mwandishi Wetu, BrotherDanny BlogArusha: JUMLA  ya ajali 10,586  zilitokea kwa kipindi cha Januari hadi Agosti 2014 ambapo ajali hizo ni pungufu  kwa ajali 5,096 ikilinganishwa na ajali 15 ,682 zilizotokea kati ya Januari hadi Agosti 2013.
Aidha, kati ya ajali hizo madhara ya vifo na majeruhi yamepungua ambapo vifo vimepungua kwa watu 40 huku majeruhi yakipungua hadi 3,603.


Hayo yalisemwa jana na Katibu wa Baraza la Usalama Barabarani Mohamed Mpinga alipokuwa akiongea na waandishi wa habari kuhusiana na hali ya ajali hapa nchini katika Wiki ya Nenda kwa Usalama ambayo bado inaendelea jijini hapa.
Mpinga alisema kuwa ajali hizo zinatokana na uzembe na makosa mbali mbali wanayoyafanya madereva na kwamba jitihada zote hizo za kupungua kwa idadi ya ajali hizo zimetokana na jeshi kutoa mbinu kwa madereva za kuwafanya waweze kuepuka ajali zinazokwepeka.
Aidha, alitaja ajali zilizohusisha pikipiki kwa kipindi cha Januari hadi Agosti 2013 kuwa ni ajali 4,467 wakati waliofariki ni watu 704 na waliojeruhiwa wakiwa ni watu 4,312.
Alileleza kuwa kwa mwaka 2014 ajali za pikipiki zimepungua hadi kufikia 3,998 vifo navyo vikiwa vimepungua kwa kufikia 608 huku majeruhi wakiwa 2,883.
Aliongeza kuwa katika udhibiti wa ukamataji wa  makosa  ya usalama barabarani kwa 2014 walifanikiwa kukamata makosa 67,635 ambapo mwezi Agosti yalipanda na kufikia 102,505 ikiwa ni ongezeko la makosa 34,870 sawa na asilimia 52.
Hata hivyo, alisema kuwa jeshi la polisi linaendelea na kutoa elimu zaid kwa madereva na wananchi ili kuhakikisha kuwa ajali zinazoua watu kutokana na uzembe wa barabarani zinazidi kupungua zaidi.

No comments:

Post a Comment