Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Sunday 28 September 2014

HURUMA, MAADILI MABAYA CHANZO CHA AJALI BARABARANI

Mojawapo ya ajali za barabarani zilizotokea mwezi Agosti mwaka huu

Na Mwandishi Wetu, BrotherDanny BlogArusha: IMEELEZWA kuwa baadhi ya ajali ambazo zinatokea barabarani wakati mwingine zinasababishwa na huruma pamoja na maadili mabaya ya baadhi ya askari wa kikosi cha usalama barabarani hali ambayo pia inaongeza vifo.
Hata hivyo huruma hizo ambazo zinatoka kwa askari hao pamoja na maadili mabaya pia chanzo chake ni maslahi duni ambayo wanayapata pamoja na ugumu wa kazi katika vituo vyao.


Hayo yameelezwa jana na Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Erasto Mbwilo wakati akifunga rasmi wiki ya usalama barabarani iliyokuwa ikifanyika kitaifa mjini Arusha.
Mbilo alisema kuwa ni dhairi kwa baadhi ya askari wa usalama barabarani kuwa wanajikuta wakiwa wanaona huruma kwa waalifu wa makosa ya barabarani ili waweze kupewa hongo kidogo ambapo pia hongo hiyo huwasaidia kujikimu kwa siku.
Alieleza hali hiyo inachangia sana vifo visivyo na lazima kutokea kutokana na baadhi ya madereva kujikuta wakiwa wanatenga fedha za kuwapa maaskari ili hali wanavunja na kuharibu sheria za barabarani tena kwa kujua.
"Huu ni wakati sasa wa kuona chanzo cha ajali nyingi ni nini mimi nadhani kuwa ni huruma ya baadhi ya askari wetu lakini hata wale ambao hawana huruma wengi wao pia hawana maadili ni jukumu la baraza la usalama barabarani kuliangalia hili na kisha kulitatua hawa askari wanateseka sana barabarani sasa kwa nini wasichukue au kutamani hata elfu moja," aliongeza Mbwilo.
Wakati huo huo alidai kuwa nao askari wa kikosi hicho cha usalama hawapaswi kusingizia kuwa wanachukua rushwa kuanzia shilingi mia tano na kuendelea kwa kisingizio kuwa maisha ni magumu bali wanatakiwa kuangalia maadili ya kazi na kisha kuwachukulia sheria baadhi ya madereva ambao ni wazembe barabarani.
Katika hatua nyingine alisema kuwa nao viongozi hasa wale wa Serikali hawapaswi kuwa chanzo cha kuvunja sheria za barabarani kwa kuwaharakisha madereva wao kuwai na badala yake wanatakiwa kuwa mfano bora kwenye jamii kwa kusisitiza umuhimu wa kufuata sheria za barabarani.
Naye Katibu wa Baraza la Usalama Barabarani Mohamed Mpinga alisema kuwa ya ajali 10,586  zilitokea kwa kipindi cha Januari hadi Agosti 2014 ambapo ajali hizo ni pungufu  kwa ajali 5,096 ikilinganishwa na ajali 15 ,682 zilizotokea kati ya Januari hadi Agosti 2013.
Mpinga alimalizia kwa kusema kuwa pamoja na kuwa wamefanikiwa kwa kiwango kikubwa kupunguza wimbi la ajali za barabarani lakini bado baraza hilo linakabiliwa na changamoto ya uhaba wa bajeti hivyo kuna umuhimu wa kuongeza bajeti hiyo ili kufanikisha zoezi la kupunguza ajali.

No comments:

Post a Comment