Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Friday 26 September 2014

SERENGETI FIESTA SONGEA KWA MARA YA KWANZA


Baada ya kushusha burudani ya aina yake katika mikoa ya Iringa na Morogoro wiki iliyopita, Tamasha la Serengeti Fiesta 2014 linaendelea na sasa limejipanga kwa ajili ya kuwasha moto kwa wakazi wa mji wa Songea na viunga vyake kwa mara ya kwanza katika historia ya tamasha hilo nchini. Burudani hiyo ya kihistoria itafanyika leo katika Uwanja wa Majimaji mjini humo.
Kila kitu kipo sawa kwa upande wa kampuni ya bia ya Serengeti ambao ndio wadhamini wakuu wa shoo na safari zote za Serengeti Fiesta mwaka huu ambazo zimekuwa za mafanikio makubwa, ziara za tamasha hilo zinakaribia kufika kikomo chake hapo Oktoba 18.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa waandaaji wa tamasha hilo, wasanii wanaotarajiwa kutoa shoo katika Uwanja wa Majimaji mjini Songea leo ni pamoja na Godzilla, TID, Linex, Mr. Blue, Madee, Stamina, Barnaba, Ney wa Mitego, Linah, Recho, Mo Music na Baraka Da Prince.
Kabla ya wasanii hao kupanda jukwaani na kutoa shoo usiku huu, baadhi ya shughuli mbalimbali zitafanyika ikiwemo Serengeti Super nyota diva. Shughuli yenye lengo la kumtafuta mwanadada mwenye kipaji cha kuimba toka katika mji huo wa Songea ili aje kushuhudia tamasha la mwisho jijini Dar es Salaam. Lengo la Serengeti katika shughuli hiyo ni kuwasaidia vijana na kuendeleza vipaji vyao kama ilivyokuwa kwa Young Killer.    
Wakati maandalizi ya shoo yakikaribia, Meneja wa kinywaji mama cha Serengeti Premium Lager, Ndugu Rugambo Rodney alizungumza na waandishi wa habari na kusema......“Songea ni mkoa ambao Serengeti Fiesta inapita kwa mara ya kwanza katika historia ya maonyesho ya tamasha hili nchini Tanzania..... napenda kuwajulisha wakazi wa Songea kwamba shoo zetu ni za pekee na kwamba tupo tayari ku “Sambaza Upendo” leo katika mkoa wao. Pia nataka kuwahakikishia kwamba tutatoa shoo bora na nzuri ambayo hamjawahi kuiona katika mkoa wenu, tunatarajia mtajitokeza kwa wingi kushuhudia baadhi ya wasanii ambao hawajawaji kutoa burudani katika mkoa wenu.”
Katika kuliweka wazi suala la ulinzi uwanjani hapo, Rodney alisema “Walinzi watakuwepo kila eneo uwanjani hapo kama ambavyo ilikuwa katika shoo zilizopita.”

Songea utakuwa mkoa wa 13 ambao tamasha hilo la Serengeti Fiesta limepita na kufanya shoo zake kwa mwaka huu. Mtwara, Mbeya, Dodoma na Dar es Salaam ni mikoa ambayo inasubiri kwa hamu kuonja ladha ya tamasha hilo lililojizolea umaarufu toka kila kona ya mikoa ambayo limepita.

No comments:

Post a Comment