Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Saturday 6 September 2014

MAKUNGA ASTAAFU MWANANCHI


Theophil Makunga, ndiye mhariri mwanzilishi wa gazeti la Mwananchi

Dar es Salaam. Mhariri Mtendaji Mkuu wa kwanza na mwanzilishi wa Gazeti la Mwananchi, Theophil Makunga amestaafu kuitumikia Kampuni ya Mwananchi Communications Limited (MCL).
MCL ndiyo kampuni inayochapisha magazeti ya Mwananchi, The Citizen na Mwanaspoti, chini ya Kampuni ya Nation Media Group yenye makao makuu yake Nairobi, nchini Kenya.
Makunga amestaafu MCL, baada ya kuitumikia kwa mafanikio makubwa kwa zaidi ya miaka 14 katika nyadhifa mbalimbali za uongozi, tangu kuanzishwa kwake mwaka 2000.
Sherehe ya kumuaga Makunga iliyoandaliwa na MCL, ilifanyika juzi jioni kwenye Hoteli ya Serena, iliyoenda sanjari na kusherehekea siku ya kuzaliwa kwake, ambapo alikata keki akishirikiana na mkewe, Wilhelmina pamoja na mwanaye wa kwanza.
Hadi anastaafu MCL, Makunga alikuwa Meneja Uendelezaji Biashara.
Alipopewa fursa ya kuzungumza alisema: “Sijui nianzie wapi...lakini Mungu ndiye anajua. Maisha yangu na Mwananchi ya miaka kumi na mitano, yataendelea hivyohivyo.
“Mimi nafikiri Mwananchi kuna damu yangu kutokana na tulivyoanza mpaka sasa,” alisema Makunga ambaye alikuwa akitoa shuhuda mbalimbali alizokutana nazo kubwa ikiwa ni milipuko ya mabomu kambi ya Jeshi la Wananchi(JWTZ), Gongo la Mboto.
Aliongeza:“Sitafanya kitu kitachochanganya damu yangu. Nitakuwa tayari kutoa ushauri wowote, nashukuru kwa kuishi nanyi pamoja, ngoja nikajaribu maisha ya kustaafu yanakuwaje.”
Akizungumzia historia yake na waanzilishi wenzake, Makunga alisema, walikuwa wanne lakini wamebaki wawili huku wawili wakiwa tayari wamefariki dunia na sasa aliyebaki katika fani ya habari MCL ni mmoja.
Alibainisha kuwa alikuwa yeye (Makunga), Julius Magodi ambaye ndiye aliyebaki MCL mpaka sasa, huku Danny Mwakiteleko na Conrad Dustan aliyemwita ‘kiona mbali’ wakiwa ni marehemu.
“Vijana, MCL ni sehemu nzuri pa kufanya kazi, lakini natoa ushauri kwa MCL kuandaa mpango wa kuwa na mafunzo maalumu kwa wafanyakazi wake wanaotaka kustaafu ili kuwajengea uwezo kuanza maisha mapya,” alisema.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa MCL, Francis Nanai alisema: “Tendo hili linaumiza, lakini kwa niaba ya wafanyakazi wa MCL, Nation Media Group (NMG), tunakupongeza kwa kazi nzuri uliyoifanya.”
Alisema katika kila sehemu huwa kuna wafanyakazi, lakini Makunga alijitoa zaidi ya wengine kuhakikisha Mwananchi inang’ara kwa bidhaa zake.
“Unastaafu, siyo kwamba wewe ni mzee...: MCL na NMG tutaendelea kukutumia kwa baadhi ya maeneo kwani bado tunakuhitaji,” alisema Nanai na kuongeza:
“Makunga amekamilika, siyo tu mwanahabari, bali pia ni mfanyabiashara. Hivyo, mimi nakuomba usikae tu nyumbani, utafute vyuo vya habari ufundishe, hata kama ni kwa muda mfupi. Hazina uliyonayo uiache na kwa wengine.”
Alisema siyo kufundisha pekee bali Makunga aandike hata kitabu cha maisha yake ndani ya tasnia ya habari hasa akiwa MCL na kwamba, akishindwa kutokana na fedha wataangalia jinsi ya kumsaidia.
Naye Mhariri Mtendaji Mkuu wa MCL, Bakari Machumu, alisema Makunga alikuwa zaidi ya mwandishi wa habari kutokana na kuwa mbunifu wa masuala ya biashara.
“Makunga licha ya kuhama chumba cha habari, alianzisha kitengo cha ‘Breaking News’, akiwa hana bajeti wala mpango mkakati wa biashara, lakini mwezi mmoja tu, tumeona matunda yake,” alisema Machumu na kuongeza:
“Hata uzalishaji wa magazeti Kanda ya Ziwa ni matunda ya Makunga. Kuna vitu vingine hujifunzi darasani, bali unavyoishi na watu, mimi nimejifunza mengi kutoka kwake.”
Mhariri Mtendaji wa Gazeti la Mwananchi, Frank Sanga alisema kuwa katika mafanikio yake ya tasnia ya habari mtu wa kwanza anayestahili kubeba sifa hizo ni Makunga.
Alisema Januari 5 mwaka 2004, alijiunga Mwananchi kama Mhariri wa Mwanaspoti, lakini Makunga alimlea kama mtoto wake.
Kwa upande wake, Mhariri Mtendaji wa Gazeti la The Citizen, Richard Mgamba alizungumza kwa hisia, huku akitumia kitambaa kufuta machozi yaliyomtiririka.
“Makunga tunamuaga akiwa amevaa nguo na tabasamu lake tunaliona. Bado tunakuhitaji, ukienda kwa wapinzani, tutakuombea gari lako lisiwake au liharibike matairi.
Sijawahi kumwona Makunga akiwa amekasirika hali iliyotokana na moyo wake, lakini pia ni mcha Mungu. Zaburi inasema; Nimrudishie nini bwana kwa wema ulionitendea. Nami sina cha kukulipa,”alisema Mgamba.

No comments:

Post a Comment