Mwakilishi
Mkazi msaidizi kutoka UNFPA Bi. Christine Mwanukuzi akifungua mdahalo
huo, kuwashukuru vijana kwa kujumuika pamoja na kuwapongeza kwa
kufanikisha mdahalo huo kuelekea katika siku ya vijana duniani siku ya
tarehe 12.08.2016.
Bw.
Badru Juma Rajabu akielezea historia ya siku ya vijana ilipoanzia na
kusisitiza kuwa vijana wanatakiwa kutambulika na wasisahau kuchukua
fursa pale wanapowezeshwa
Oscar
Kimario muwezeshaji kutoka Restless Development akielezea baadhi ya
ripoti juu ya vijana na kuwasihi vijana kuwa ndio watakuwa mstari wa
mbele katika maendeleo endelevu hivyo wanapaswa kujituma na kufanya kazi
kwa bidii
Vijana wakiendelea kufuatilia mdahalo huo kwa makini
Mwakilishi
kutoka Shirika la Kazi la Umoja wa Mataifa ILO Nancy Lazaro
akizungumzia ajira zenye staha ,alisema kuwa vijana wengi wameajiriwa
lakini katika ajira zisizo na staha na kusisitiza ifike kipindi sasa
vijana waajiliwe na kazi zenye Staha.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Msichana Initiatives Rebeca Gyumi akijibu maswali
mbalimbali ambayo waliuliza vijana waliofika katika kongamano hilo na
kusema kwamba sio kweli kwamba wanafunzi waliomaliza elimu ya vyuo ni
vilaza
Vijana wakiendelea kufuatilia wajibu maswali wakijibu yale waliyo yauliza
Mwanafunzi
wa Shule ya Sekondari ya St.Josephs Veronica Shayo kidato cha tano
akisisitiza vijana kuwa na tabia za kuweka akiba kwa kile wanachopata
ili kije kuwasaidia pindi watakapo kuwa wakubwa.
Muwezeshaji
wakati wa kongamano hilo la vijana ambalo kauli mbiu yake inasema
Sepesha Umasikini kwa Michongo Endelevu na yenye tija Bw. Lawrence
Ambokile akiendelea kutoa mwongozo
Noreen
Toroka akijibu baadhi ya maswali lakini pamoja na hayo amewasisitiza
vijana kuto kutumia kipato wanacho kipata bila tija na wawe na utaratibu
wa kuhifadhi kwa ajili ya maendeleo baadae, pia aliongeza kuwa vijana
wasilazie damu fursa mbalimbali zinazotolewa kwa ajili yao
Baadhi ya vijana kutoka Restless Development na wanafunzi pamoja na wadau wakendelea kufuatilia mdahalo
Mwanzilishi wa Malkia Investment Bi. Jenipher Shigoli akichangia jambo katika mdahalo huo
Albert Kutoka ILO akichangia na kujibu maswali ya vijana mbalimbali katika mdahalo huo ambapo alisisitiza vijana kujituma
Mwanzilishi
wa Charity Movement Sophia Mbeyela akitoa ushuhuda wake wa jinsi alivyo
anza ujasiliamali tangia akiwa mdogo na kusisitiza kwamba vijana
haijalishi ni mzima au ana ulemavu wa viungo vya mwili wake wote
wanatakiwa kujumuika pamoja na kufanya kazi kwa bidii ili kuleta
maendeleo ya Taifa
Kijana Onesmo akiwaeleza vijana wenzake kuwa kama wao walemavu wa viungo wanaweza kufanya mambo makubwa iwEje vijana wazima wasiweze hii ilikuwa ni changamoto
Picha ya pamoja ya Baadhi ya Washiriki wa Mdahalo huo
Picha na Fredy Njeje wa Blogs za Mikoa
No comments:
Post a Comment