Meneja
Miradi wa Tigo, Anthony Njau (katikati), akizungumza katika mkutano na
waandishi wa habari Makao Makuu ya Tigo Dar es Salaam leo aasubuhi
kuhusu kampuni hiyo na Kampuni ya ya Kupatana.com, kushirikiana
kuwezesha biashara kwa mtandao. Kulia ni Mkurugenzi wa Kampuni ya
Kupatana.com, Philip Ebbersten na kushoto ni Meneja Mkazi wa Kampuni
hiyo, Makusaro Tesha.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Kupatana.com, Philip Ebbersten (kulia), akizungumza kwenye mkutano huo.
Meneja Mkazi wa Kampuni hiyo, Makusaro Tesha (kushoto), akizungumza katika mkutano huo.
Mkutano na wanahabari ukiendelea.
Na Dotto Mwaibale
Kampuni
inayoongoza kwa mtindo wa maisha ya kidijitali Tigo Tanzania na kampuni
ya Kupatana.com, moja ya kampuni zinazoongoza Tanzania katika huduma
za masoko katika mtandao zimeingia katika ubia wa kibiashara ambapo
kila kampuni itauza bidhaa na huduma za kila mmoja katika majukwaa yao
ya kidijitali.
Katika
hatua za mwanzo za ushirikiano huu, Kampuni ya Tigo Tanzania itachagua
maduka matatu ambayo Kupatana.Com itayatumia kuwawezesha wateja wa Tigo
kuuza simu zao zilizotumika kwa kupitia jukwaa la Kupatana.com.
Akizungumza
wakati wa kusaini makubaliano baina ya pande hizo mbili jijini Dar es
Salaam, Meneja wa Miradi wa Kampuni ya Tigo, Anthony Njau alisema,
“tukiwa ni kampuni ya mtindo wa maisha ya kidijitali, tumeona kwamba
hivi sasa Watanzania wamehamasika mno katika kufanya biashara kupitia
njia ya mtandao.”Njau aliongeza kwamba , “Mtandao na wavuti wa
Kupatana.com unatoa jukwaa zuri ambalo linabadilisha namna ambavyo watu
wanaishi kwa kuwezesha kupatikana kwa huduma na bidhaa katika njia
sahihi na rahisi.”
“Lengo
la muda mrefu ni kuwapatia wateja wetu jukwaa ambalo wanaweza kupakua
vifaa ambavyo vilishatumika ili kuviboresha na kwa upande wa Tigo kuuza
vifaa vipya, kuongeza usambazaji na kuwa na mafanikio katika jaribio
hili la msingi, Tigo na Kupatana.com zitapanua wigo wa huduma hii na
kuhakikisha inapatikana kwa urahisi katika maduka yote 52 ya Tigo
ambayo yamesambaa kote nchini,” alisema Njau.
Mkurugenzi
wa Kupatana.com, Philip Ebbersten, alisema kwamba kupitia matumizi ya
jukwaa hilo, wauzaji (kampuni na watu binafsi) wataweza kuwafikia
maelfu ya wanunuzi muhimu kila siku bila kujali maeneo yao ya
kijiografia.
Alifafanua
kuwa kuorodhesha bidhaa katika jukwaa hilo ni bure na kuwashauru
wateja umuhimu wa kufuata kanuni na miongozo salama kwa bidhaa zote
zitakazotangazwa Kupatana.com ili waweze kuzitapa kwa usalama na uelewa
zaidi.
No comments:
Post a Comment