Mkurugenzi
wa Sensa na Takwimu za Jamii wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS),
Ephraim Kwekisigabo (kulia), akizungumza katika mkutano na waandishi wa
habari Dar es Salaam leo, wakati akitoa taarifa za mfumuko wa bei wa
taifa wa mwezi Julai, 2016. Kushoto ni Kaimu Meneja, Idara ya Takwimu ya
Ajira na Bei, Ruth Minja.
Mkutano na wanahabari ukiendelea.
Wapiga picha wakiwa kazini.
Na Dotto Mwaibale
MFUMUKO wa Bei wa Taifa kwa mwezi Julai, 2016 umepungua hadi asilimia 5.1 kutoka asilimia 5.5 ilivyokuwa mwezi Juni, 2016.
Hayo
yamebainishwa na Mkurugenzi wa Sensa na Takwimu za Jamii wa Ofisi ya
Taifa ya Takwimu (NBS), Ephraim Kwekisigabo wakati akizungumza katika
mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo kuhusu mfumuko wa bei
wa taifa wa mwezi Julai, 2016.
"Hii
inamaanisha kuwa kasi ya upandaji wa bei za bidhaa na huduma kwa mwaka
ulioishia mwezi Julai, 2016 imepungua ikilinganishwa na kasi iliyokuwepo
kwa mwaka ulioishia mwezi Juni 2016" alisema Kwesigwabo.
Kwesigabo
alisema kuwa Fahirisi za Bei zimeongezeka hadi 103.50 Mwezi Julai, 2016
kutoka 98.48 mwezi Julai 2015 na kuwa mfumuko wa bei za bidhaa za
vyakula na vinywaji baridi mwezi Julai 2016 umepungua hadi asilimia 7.6
kutoka asilimia 8.1 ilivyokuwa mwezi Juni, 2016.
Kwesigabo
aliongeza kuwa kupungua kwa mfumuko huo wa bei wa mwezi Julai 2016
kumechangiwa na kupungua kwa kasi ya bei za baadhi ya bidhaa za vyakula
na zisizo za vyakula kwa kipindi kilichoishia mwezi Julai, 2016
zikilinganishwa na bei za mwezi Julai 2015.
Alisema
mwenendo wa bei za baadhi ya bidhaa za vyakula zilionesha kupungua ni
pamoja na bei za samaki kwa asilimia 6.6, mafuta ya kupikia kwa asilimia
4.9 na maharage kwa asilimia 1.9.
Aliongeza
kuwa kwa upande mwingine mwenendo wa bei za baadhi ya bidhaa ziliso za
vyakula zilionesha kupungua ni pamoja na bei za gesi kwa asilimia 21.5,
mafuta ya taa kwa asilimia 9.4 na dizeli kwa asilimia 10.3
Alisema
pamoja na kupungua kwa kasi ya upandaji wa bei za bidhaa na huduma kwa
mwaka ulioishia mwezi Julai, 2016 kuna baadhi ya bidhaa zilionesha
kuongezeka katika kipindi hicho zikiwa ni pamoja na bei za mchele kwa
asilimia 4.7, mahindi kwa asilimia 31.6, unga wa mahindi kwa asilimia
24.1, vyakula kwenye migahawa kwa asilimia 15.6 na mkaa kwa asilimia
16.0.
No comments:
Post a Comment