Kaimu Mkurugenzi wa Utafiti
na Uchimbaji wa Shirika la Madini (STAMICO) Alex Rutagwelela (Katikati)
akiongea na waandishi wa Habari (Hawapo pichani) wakati wa maonyesho ya
Nane nane Viwanya vya Ngongo - Lindi.
Katika
kuhakikisha wachimbaji wadogo wananufaika na kazi zao na kuepuka
kuondolewa na wachimbaji wakubwa wameshauriwa kuchukua leseni ndogo za
awali za uchimbaji.
Wito
huo kwa wachimbaji umetolewa na kaimu mkurugenzi wa utafiti na
uchimbaji wa shirika la madini (STAMICO) Alex Rutagwelela alipokuwa
anazungumza na waandishi wa habari katika viwanja vya ngongo Manispaa ya
Lindi yanapofanyika maonyesho ya nane nane kitaifa.
Rutagwelela
alisema wachimbaji wadogo wanatakiwa kuwa na leseni za awali
zitakazowafanya wawe na haki kwenye maeneo wanayochimba. hivyo kuwa na
uhakika wa kuto ondolewa bila taratibu na wachimbaji wakubwa kwenye
maeneo wanayochimba.
Wananchi
wakisikiliza maelekezo kutoka kwa Maafisa wa STAMICO walipotembelea
Banda lao katika Maonyesho ya Nane nane yanayoendelea Mkoani Lindi
katika viwanja vya Ngongo.
Aliwahakikishia
wanahabari na wananchi shirika hilo linania ya kuwainua wachimbaji
wadogo kwa kufanyia tathimini maeneo wanayochimba ili waweze kujua kiasi
cha madini na mashapo yaliyopo katika maeneo hayo.
Alisema
wachimbaji wanaweza kupata fursa ya mafunzo ili waweze kupata ujuzi wa
kuyafahamu mambo ya kijiolojia, vilevile watakuwa na uwezo wa kupata
mikopo.
Hata hivyo alitahadharisha kwamba wanaweza kunufaika na fursa hizo ni wachimbaji wenye leseni.
"Wachimbaji
wenye leseni nilazima wainuliwe, wengi wao hawana mitaji wanachimba
kipindi cha masika kwenye makorongo na kiasi wanachopata ni kidogo sana,
kwamfano wilaya ya Ruangwa na mkoa huu unamadini ya aina nyingi na
mengi wakiwezeshwa watanufaika," alisema Rutagwelela.
Akibainisha
wachimbaji wadogo wanachimba kwa kubahatisha, hivyo shirika hilo
lipotayari kuwasaidia kufanya tathimini na kuwaonesha kiasi cha mashapo
yaliyopo katika maeneo wanayochimba.
Huku akitoa wito wawe tayari kwa uchangiaji kiasi kidogo cha fedha ambacho ni rafiki kwa wachimbaji wadogo kwa ajili ya gharama ya uendeshaji mitambo wakati wa kuchoronga, ikiwamo mafuta.
Akiongeza kusema STAMICO kwa niaba ya serikali imejipanga kuwasaidia kufikia malengo yao ya kiuchumi na kimaendeleo.
Huku akitoa wito wawe tayari kwa uchangiaji kiasi kidogo cha fedha ambacho ni rafiki kwa wachimbaji wadogo kwa ajili ya gharama ya uendeshaji mitambo wakati wa kuchoronga, ikiwamo mafuta.
Akiongeza kusema STAMICO kwa niaba ya serikali imejipanga kuwasaidia kufikia malengo yao ya kiuchumi na kimaendeleo.
No comments:
Post a Comment