Naibu waziri Ofisi ya Rais
Tawala za Mikoa na serikali za mitaa TAMISEMI Jafo Suleiman Said akisalimiana
na Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Miraji Jumanne Mtaturu mara baada ya kuwasili
katika uwanja wa maonesho ya nane nane Nzuguni mjini Dodoma.
Naibu waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na serikali za mitaa TAMISEMI Jafo Suleiman Said akisikiliza kwa makini maelezo ya kilimo cha mbogamboga yanayofanywa na Jeshi la kujenga Taifa JKT.
Naibu waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Jafo Suleiman Said akiwa kwenye picha ya pamoja na watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama mara baada ya kutembelea banda la Halmashauri hiyo.
Naibu waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na serikali za mitaa TAMISEMI Jafo Suleiman Said akisikiliza kwa makini maelezo ya awali kutoka kwa Mwenyeji wake katika Maonesho hayo ambaye ni mkuu wa Wilaya ya ikungi Miraji Jumanne Mtaturu.
Naibu waziri TAMISEMI Jafo Suleiman Said akisaini kitabu cha wageni katika banda la Mwanzo Bora Nutrition Program.
Mgeni na Mwenyeji wakifurahi kufuatia maandalizi mazuri ya Maonesho ya Nane nane kanda ya kati.
Naibu waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na serikali za mitaa TAMISEMI Jafo Suleiman Said akisikiliza kwa makini maelezo ya kilimo cha mbogamboga yanayofanywa na Jeshi la kujenga Taifa JKT.
Naibu waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Jafo Suleiman Said akiwa kwenye picha ya pamoja na watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama mara baada ya kutembelea banda la Halmashauri hiyo.
Naibu waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na serikali za mitaa TAMISEMI Jafo Suleiman Said akisikiliza kwa makini maelezo ya awali kutoka kwa Mwenyeji wake katika Maonesho hayo ambaye ni mkuu wa Wilaya ya ikungi Miraji Jumanne Mtaturu.
Naibu waziri TAMISEMI Jafo Suleiman Said akisaini kitabu cha wageni katika banda la Mwanzo Bora Nutrition Program.
Mgeni na Mwenyeji wakifurahi kufuatia maandalizi mazuri ya Maonesho ya Nane nane kanda ya kati.
Naibu waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na serikali za mitaa TAMISEMI Jafo Suleiman Said akisikiliza maelezo ya namna ya kulima kilimo na ufugaji wa kisasa.
Naibu waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na serikali za mitaa TAMISEMI Jafo Suleiman Said akizungumza na Luteni AJ Massawe Meneja wa banda la JKT.
Naibu waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na serikali za mitaa TAMISEMI Jafo Suleiman Said akipokea zawadi ya mafuta ya alizeti kutoka kwa Mkuu wa Wilaya ya Kongwa Deogratius Ndejembi.
Naibu waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na serikali za mitaa TAMISEMI Jafo Suleiman Said akiwa katika pichaya pamoja na Mkuu wa Wilaya ya ikungi na Kongwa pamoja na watendaji Mfuko wa LAPF.
Na Mathias
Canal, Dodoma
Watanzania wametakiwa kuthamini na kununua bidhaa
zinazozalishwa nchini Tanzania hususani katika sekta ya Kilimo, Ufugaji na
uvuvi kwani hakuna sababu ya kuagiza bidhaa kutoka nje ya nchi ilihali bidhaa
hizo wanazoagiza zinazalishwa na watanzania wenzao.
Naibu waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na
serikali za mitaa TAMISEMI Jafo Suleiman
Said ameyasema hayo mara baada ya kutembelea baadhi ya mabanda katika
maonyesho ya wakulima Nane nane Kanda ya kati Dodoma yanayofanyika katika
uwanja wa Nzuguni huku kauli mbiu ya mwaka huu ikiwa ni "Kilimo, Mifugo na
Uvuvi ni nguzo ya maendeleo, Kijana shiriki kikamilifu (Hapa Kazi Tu).
Jaffo amesema kuwa asilimia
kubwa ya watanzania wamekuwa watumwa wa mambo ya kigeni, kuiga tamaduni
mbalimbali ikiwemo matumizi ya bidhaa zinazotoka nje ya nchi wakati pia bidhaa
hizo zinazalishwa nchini, huku akitolea mfano wa manunuzi ya viatu kutoka nchi
mbalimbali wakati hapa nchini Jeshi la Magereza linatengeneza viatu bora vya
ngozi tena kwa bei nafuu.
Sambamba na hayo pia Naibu Waziri huyo ameiagiza
Mamlaka ya Ustawishaji Makao makuu Dodoma kusimamia vyema na kwenda na kasi
kubwa katika utengenezaji wa stendi kubwa na ya kisasa ili kufanana na mji wa
Dodoma ambapo pia hivi karibuni makao makuu ya serikali yatahamia mjini hapo.
Aidha ameongeza kuwa Maonesho hayo yanapaswa
kuboreshwa ili maonyesho yajayo yawe ya kitaifa ambapo nchi mbalimbali zitapata
fursa ya kutembelea na kuifanya Tanzania kujikomboa katika wimbi la umasikini.
Maonesho hayo yanahusisha Shughuli za wakulima,
wafugaji wa mifugo, wafugaji wa nyuki, wavuvi, wana mazingira, wasindikaji wa
bidhaa za mazao ya kilimo na mifugo, wizara taasisi/Makampuni ya umma,
makampuni Binafsi, mabenki, taasisi za umma na za binafsi na mashirika yasiyo
ya kiserikali.
Akitoa salamu za shukrani kwa niaba ya waandaaji
wa Maonesho hayo Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mkoani Singida Miraji Jumanne Mtaturu amesema kuwa maandalizi ya maonyesho hayo
yametumia muda mfupi lakini kwa kiasi kikubwa yamekuwa bora na kuahidi kuwa na
Maonesho yajayo kuwa bora zaidi katika kipindi kinachokuja.
Mtaturu amesema kuwa lengo mahususi la maonesho
hayo ni utoaji wa elimu ya matumizi ya teknolojia mbalimbali kwa wadau wengi
kwa muda mfupi ambapo watajifunza kwa njia ya kuona, kujadiliana na kuulizana
maswali.
Ameongeza kuwa maeneo makuu ya mafunzo ni
teknolojia za uzalishaji wenye tija wa mazao, mifugo na usindikaji wa bidhaa
ili kuongeza thamani.
Dc Mtaturu amesema kuwa pia wadau
watajionea na kujifunza huduma zitolewazo na serikali, Mashirika ya umma na
binafsi, ambapo wafanya biashara wanayatumia maonesho hayo kwa kuuza bidhaa,
kufahamiana na kuingia makubaliano.
Kwa upande wake Katibu wa maandalizi ya Maonesho
hayo Aziza Rajabu Mumba amesema kuwa
Wanatarajia kila mwananchi atakayetembelea maonesho hayo kwenda kutekeleza kwa
vitendo anayojifunza katika eneo lake na kuwafundisha wengine ambao hawakupata
fursa ya kuhudhuria kwenye Maonesho hayo.
Aidha amesema Malengo ya muda mrefu ni kuendeleza
uwanja wa Nzuguni ufikie ubora na hadhi ya viwanja vya maonesho ya Kilimo
Kimataifa na kuendelea kushawishi wadau mbalimbali kuwekeza ili kuufanya uwanja
wa Nzuguni uwe kituo cha huduma cha Maonesho ya Kilimo nchini kama ilivyo kwa
uwanja wa Mwalimu Nyerere Dar es salaam kwa maonesho ya Biashara.
No comments:
Post a Comment