Meneja Mkuu wa TV 1, Joseph Sayi (katikati), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo, kuhusu ,Kituo cha Televisheni cha TV1 Tanzania kuanza kurusha matangazo ya moja kwa moja ya mpira wa miguu ya ligi kuu soka ya Uingereza EPL matangazo ambayo yanatarajia kurushwa kuanzia Agosti 13 mwaka huu. Kulia ni Meneja Masoko wa TV 1, Gillian Rugumamu na Meneja Masoko Startimes Felix Awino.
Meneja Masoko wa TV1, Bi. Gillian Rugumamu, akifafanua jambo kuhusu uamuzi wa kituo hicho kurusha bure matangazo ya kandanda ya Ligi Kuu ya England kuanzia wiki ijayo. Kushoto ni Meneja Mkuu wa kituo hicho, Joseph Sayi, na kulia ni mchambuzi wa masuala ya soka nchini Dk. Leakey Abdallah.
Mchambuzi wa Michezo Dk. Leakey Abdallah (katikati), akizungumzia masuala ya mpira katika mkutano huo.
Meneja Uzalishaji wa TV1, Mukhsin Khalfan Mambo akizungumza katika mkutano huo.
Mkutano ukiendelea.
Wanahabari wakiwa kazini.
Taswira ya meza kuu katika mkutano huo.
Mtangazaji wa michezo wa TV1, Ally Kashushu (kushoto) ambaye ndiye atakayeendesha kipindi cha Kandanda la Premier League, akifafanua jambo katika mkutano na wanahabari.
Mmiliki wa Blog ya Kajuna Son, Cathbert Kajuna (kulia), akiuliza swali katika mkutano huo.
Wapiga picha za habari wakiwa kazini.
Baadhi ya wafanyakazi wa TV 1 wakiwa wakifuatilia matukio mbalimbali ya mkutano.
Mkutano ukiendelea.
Meneja Uzalishaji wa TV1, Mukhsin Mambo,
akionyesha studio ambayo itatumika kurushia matangazo ya Ligi Kuu England
kuanzia Agosti 10, 2016 hadi msimu wa ligi utakapomalizika Mei 2017.
Mtangazaji wa michezo wa TV1, Ally Kashushu (kushoto) ambaye ndiye atakayeendesha kipindi cha Kandanda la Premier League, akiwa pamoja na mchambuzi maarufu wa soka nchini, Dk. Leakey Abdallah (wa tatu kushoto) pamoja na wanahabari katika studio itakayotumika kurushia matangazo.
MAMBO yameiva! Mashabiki wa soka nchini Tanzania sasa wataona
live mechi za Ligi Kuu ya England bure kupitia Kituo cha luninga cha TV1 cha
jijini Dar es Salaam, www.brotherdanny.com
inaripoti.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam,
Meneja Masoko wa TV1, Gillian Rugumamu, amesema Watanzania watakayopata
matangazo hayo ni wale wote wenye ving’amuzi vya StarTimes, ambao
hawatalazimika kulipia gharama zaidi ya zile za kawaida za vifurushi vyao.
“Lengo letu ni kuwapatia mashabiki wa soka nchini Tanzania uhondo
na fursa ya kutazama mechi za England bure kupitia kituo chetu cha TV1,”
alisema Bi. Rugumamu.
Gillian Rugumamu alisema lengo ni kuwapelekea watazamaji wao wa Tanzania Ligi Kuu England ambayo ni ligi inayopendwa na kufuatiliwa na Watanzania.
Gillian Rugumamu alisema lengo ni kuwapelekea watazamaji wao wa Tanzania Ligi Kuu England ambayo ni ligi inayopendwa na kufuatiliwa na Watanzania.
Meneja Mkuu wa kituo hicho, Joseph Sayi, amebainisha kwamba,
wamejipanga kuwapa fursa Watanzania kwa kuonyesha mpira bure kupitia king’amuzi
cha StarTimes bila gharama za ziada ili waweze kunufaika na burudani hiyo ya
soka.
“Watanzania wanapenda sana mpira, hasa Ligi Kuu ya England na
kuna mashabiki wengi sana hapa nyumbani wa timu zinazoshiriki ligi hiyo, lakini
wanakosa fursa hiyo kwa sababu katika vituo vingine wanalazimika kulipa gharama
kubwa ili waweze kutazama, sisi hapa tutaonyesha bure,” alisema Sayi.
Kwa upande Mkuu wa Kituo cha TV 1 Tanzania Joseph Sayi alisema hii ni fursa kubwa kwa wadau wa soka hapa nchini kuishuhudia ligi hiyo moja kwa moja.
Naye Meneja Uzalishaji wa kituo hicho, Mukhsin Mambo ambaye ni mmoja wa watangazaji mahiri nchini Tanzania, amesema kwamba tayari kitengo chake imejipanga vyema kuhakikisha kinawaletea mashabiki na watazamaji wake uhondo huo kwa kuwatumia wataalamu wake wenye uzoefu wa uzalishaji wa vipindi bora ndani na nje ya Afrika.
Kwa upande Mkuu wa Kituo cha TV 1 Tanzania Joseph Sayi alisema hii ni fursa kubwa kwa wadau wa soka hapa nchini kuishuhudia ligi hiyo moja kwa moja.
Naye Meneja Uzalishaji wa kituo hicho, Mukhsin Mambo ambaye ni mmoja wa watangazaji mahiri nchini Tanzania, amesema kwamba tayari kitengo chake imejipanga vyema kuhakikisha kinawaletea mashabiki na watazamaji wake uhondo huo kwa kuwatumia wataalamu wake wenye uzoefu wa uzalishaji wa vipindi bora ndani na nje ya Afrika.
“Tunawahakikishia wateja wetu kupata viwango vya kimataifa na
uhakika kwamba uzalishaji unafanyika kwa viwango vya juu katika ubunifu,
kiufundi na uhariri kama ambavyo wameshuhudia kwenye vipindi vyetu
vinavyoendelea,” alisema Mambo.
Akifafanua Zaidi, Mambo alisema kwamba urushaji wa ligi hiyo
ya England ambao umepewa jina la ‘Kandanda la Premier League – KPL’ utafanyika
mara tatu kwa wiki kati ya Jumatano, Ijumaa na Jumamosi kuanzia Agosti 10, 2016
kwa muda wa wiki 33 za msimu mzima.
“Jumatano tutazungumzia yaliyojiri kwenye Ligi Kuu England, ambapo
kipindi hicho cha saa moja kitajadili mechi zilizochezwa wiki iliyotangulia,
wachambuzi watajadili, zitatolewa taarifa mahsusi, matokeo, msimamo wa ligi,
wachezaji, timu, makocha, waamuzi, magoli na tathmini nzima ya mechi zilizochezwa
kwa ujumla,” alisema.
Aidha, alisema kwamba, siku hiyo pia watajadili historia ya
mechi mbalimbali, wachezaji, viwanja na watazungumzia masuala ya uhamisho,
kununi na sheria mpya.
Kwa siku ya Ijumaa, alisema watajadili mechi zitakazochezwa
mwishoni mwa wiki wakati kipindi cha Jumamosi kitakachorushwa moja kwa moja kitakuwa
na mahojiano kabla ya mechi, ambapo kutakuwa na uchambuzi wa kina kwa muda
dakika 30 kabla, dakika 15 za mapumziko na dakika 30 baada ya mechi.
“Vipindi vyetu pia vitakuwa na marudio ambapo kipindi cha
Jumatano kitarudiwa Alhamisi, kipindi cha Ijumaa kitarudiwa Jumamosi asubuhi na
mpira wa moja kwa moja wa Jumamosi utarudiwa Jumapili,” alisema.
Kwa upande wake, Meneja Masoko wa kampuni ya StarTimes Limited, Felix Awino, amesema kwamba hawataweka tozo la nyongeza katika vifurushi vyao
hatua ambayo itawapa nafasi Watanzania wengi kushuhudia ligi hiyo.
“Hakuna tozo la nyongeza, ni gharama zile zile wanazolipia
sasa ndizo zitakazotumika tu,” alisema na kuwatoa shaka wapenzi wa soka nchini.
Ligi kuu soka nchini Uingereza ndio ligi maarufu zaidi duniani na hii ni kutokana na kushirikisha timu kongwe zenye ubora na mashabiki dunia nzima ikiundwa na timu maarufu duniani kama vile Manchester United, Liverpool, Arsenal pamoja na Chelsea.
TV1 Tanzania ndicho kitakuwa kituo pekee cha runinga hapa nchini kupewa haki za kurusha matangazo haya yatakayokujia moja kwa moja yaani Live yakihusisha pia uchambuzi wa ligi hiyo ambapo kutakuwa na vipindi vya kabla ya mechi na baada ya mechi husika.
Baadhi ya watangazaji na wachambuzi watakaokuwa wakishiriki katika urushaji wa matangazo hayo na uchambuzi ni Ally Kashushu na Dk. Leakey Abdallah ambaye ni mchambuzi mwenye uzoefu wa miaka 20 kwenye tasnia ya michezo husasani uchambuzi.
TV1 Tanzania ni kituo cha runinga kilianza mwaka 2013 ambapo kilianza kurusha matangazo yake rasmi Januari 2014 ambapo kimekuwa kikiandaa na kurushwa vipindi vyenye ubora wa hali ya juu ambapo TV 1 inapatikana kupitia king’amuzi cha Startimes namba 103.
No comments:
Post a Comment