Mkurugenzi Mkuu wa Airtel Bwana Sunil Colasso akiongea wakati wa
kutambulisha kuhusu Money airtel kuingia ushirikiano na NMB banki ili banki ya
NMB ihudumie wakala wa Airtel Money.
Wakala wa Airtel kupata Airtel Money salio kwenye benki ya NMB
popote
Dar es Salaam jumapili
julai 31 kampuni ya simu za mkononi
ya Airtel kupitia huduma yake inayokuwa kwa kasi ya Airtel Money imeingia ubia
na Benki ya NMB ili kutoa huduma kwa wakala wake wanaotoa huduma za Airtel
Money kujipatia huduma ya salio na pesa taslim katika matawi ya benki hiyo popote
nchini.
Akiongelea ubia huo,
Mkurugenzi wa Airtel Bw, Sunil Colaso alisema “tunachofanya Airtel na benki ya
NMB ni mundelezo wa mikakati tuliyojiwekea ya kuhakikisha tunaleta maendeleo
katika huduma za kifedha nchini ili wateja wetu wapate huduma za uhakika
na nafuu. Pia kuwepo kwa sera bora za udhibiti na uwekezaji itachochea
wawekezaji kuendelea kuboresha na kuweka miundombinu bora zaidi ya huduma ili
kugusa mahitaji ya wateja wengi”
Tunajisikia fahari kuona
NMB banki anakuwa nguzo muhimu ya kutoa huduma za Airtel Money kwa kuwafikishia
wakala wetu salio kila walipo ili waweze kuhudumia wateja wetu, hii inaonyesha
dhairi huduma za kifedha kwa mtandao zinazidi kupanuka kutokana na jitihada na
ubunifu wa watoa huduma kwa lengo la kuwahakikishia wateja usalama na
unafuu katika kufanya malipo, Nina uhakika Tanzania itaendelea kukua katika
swala la huduma za fedha endapo tu kutakuwa na mahusiano ya wadau kibiashara
kama haya ya Airtel Money na Banki ya NMB”.
“NMB itahudumia wakala wetu
zaidi ya 45,000 ili kuweka na kutoa salio la Airtel Money wakati wowote katika
matawi yao 160 nchi nzima, haya ni maendeleo makubwa sana hata kwa biashara
yetu”. alieleza Colaso
NMB na Airtel inaingia Ubia
kipindi ambacho Airtel Money pia imezindua kampeni yake kabambe ya Mr Money kwa
lengo la kuwafikishia wateja wake taarifa za uhakika na unafuu katika huduma za
Airtel Money.
Airtel Money imefanikiwa
pia kuleta huduma pekee za mikopo isiyokuwa na maharti magumu ya TIMIZA ambapo
inawawezesha wateja na mawakala wake zaidi ya milioni 2 kujipatia mikopo kila
wakati.
No comments:
Post a Comment