Twitter Buzz
....
...
IMETOSHA!
Featured post
KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO
Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...
Tuesday, 7 April 2015
NUNUENI TUMBAKU KWA MIKATABA YA KISWAHILI-WETCU
Na Hastin Liumba, TaboraCHAMA Kikuu cha Ushirika wa Wakulima wa Tumbaku kanda ya Magharibi (WETCU) kimewataka wadau wote au taasisi zinazojishughulisha na ununuzi wa zao la tumbaku kutumia mikataba ya Kiswahili na siyo kiingereza ili kuepusha migongano iliyodumu kwa muda mrefu.
Agizo hilo limetolewa na Mwenyekiti wa Bodi ya WETCU Mkandala Gabriel Mkandala katika hafla fupi iliyoandaliwa na benki ya CRDB Tawi la Tabora kwa viongozi wa vyama vya msingi,
Mkandala alisema makampuni mengi ya ununuzi wa tumbaku yanaandaa mikataba yao kwa lugha ya kiingereza lugha ambayo haifahamiki kwa wakulima wenyewe, na hili limekuwa likiwaletea migongano mingi ya kimaslahi ikiwemo kudhulumiwa pasipo kuelewa nini kilichoandikwa humo.
‘Kuanzia sasa hii mikataba inayoandikwa kwa lugha ya kiingereza hatuitaki kwa sababu wakulima wengi hawaelewi nini kilichoandikwa humo badala yake viongozi wao wanalazimishwa kukubaliana nayo tu kwa niaba ya wakulima.” aliongeza.
Wakati huo Mkuu wa Kitengo cha Mikopo wa benki ya CRDB toka Makao Makuu Patrick Alex akizungumza katika hafla hiyo aliwataka wakulima wote kuuza tumbaku yao katika vyama vyao vya msingi ili kuepusha vitendo vya ulanguzi na utoroshaji wa tumbaku hiyo na kubainisha kuwa jambo hilo ni kinyume na masharti ya mikataba yao.
Aliwataka viongozi wa vyama hivyo kuwa wazi kwa wakulima na kuwa waaminifu katika utendaji wao sambamba na vikao vya pamoja ili kubainisha changamoto zilizopo na kuweka mikakati ya kuzitatua sambamba na kuweka utaratibu mzuri utakaowasaidia kulipa madeni.
Meneja Mahusiano na Uendeshaji wa benki hiyo Albert Michael aliwataka viongozi wa vyama hivyo kukamilisha mapema taratibu zote za ujazaji mikataba kwa ajili ya maandalizi ya mikopo katika msimu ujao huku akisistiza suala zima la utunzaji kumbukumbu zao.
Naye Meneja wa Bima wa benki hiyo Arthur Mosha alielezea umuhimu wa wakulima hao kuwa na bima katika maisha yao kwa kuwa uamuzi huo ni kwa faida yao na bima hiyo itawalinda wao binafsi, watoto na mazao yao.
Awali Meneja wa benki hiyo tawi la Tabora Sydney Bakari aliwataka wakulima hao kuheshimu mikataba yao na CRDB itawapa ushirikiano mkubwa ili benki hiyo iendelee kuwahudumia zaidi na zaidi kwa lengo la kuboresha maisha yao.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment