Katika kile kinachoonekana kwamba Chama cha Mapinduzi (CCM) kimepungua ama kumalizika nguvu na mvuto, mikutano yake mingi imeonekana kukosa watu kabisa. Huu ni msafara wa Katibu wa CCM Wilaya ya Sumbawanga, Bi Lucy Mpeta, akiwa katika ziara kwenye Kijiji cha Matanga hivi karibuni.
Akina mama ndio wameendelea kuipeperusha bendera ya CCM bila kujali hata mvua zinazonyesha.
Hawa kushoto siyo abiria, ni wananchini waliojitokeza kuusubiri msafara wa Katibu wa CCM Wilaya ya Sumbawanga ambao unakaribia kuwasili mahali hapa kwa ajili ya mkutano.
Bendera zinapepea, Mwenyekiti Juuuuuu.
Kijana wa Green Guard naye akiwa makini kuhakikisha usalama, ambao ni mkubwa sana kwani amezungukwa na watoto tu waliojitokeza kwenye mikutano ya chama hicho.
Na huu ndio 'umati' wa 'wananchi' waliojitokeza kwenye mikutano ya CCM. Ni shiiiiida.
No comments:
Post a Comment