Mfalme Salman wa Saudi Arabia
Katika mageuzi ambayo hayakutarajiwa ndani ya ufalme wa Saudi Arabia, mfalme Salman amemfuta kazi kakake wa kambo Prince Muqrin ambaye alikua mrithi wa ufalme huo na badala yake akamtaja mpwae Mohammed Bin Nayef ambaye kwa sasa anashikilia wizara muhimu ya mambo ya ndani.
Mfalme huyo pia amempandisha ngazi mwanawe wa kiume Mohammed Bin Salman na kumpa cheo cha waziri wa ulinzi.
Mwana mfalme huo aliye na miaka 30 tu, sasa atakuwa ni wa pili katika orodha ya wanaotarajiwa kuurithi ufalme wa Saudia.
Uteuzi huu umefungua ukurasa mpya wa kupokeza kizazi kipya cha vijana ufalme wa nchi hiyo.
Mfalme pia ameridhia kujiuzulu kwa waziri wa mambo ya nje Saud Al Faisal, ambae ameshikilia nafasi hio kwa miongo minne.
CREDIT: BBC
No comments:
Post a Comment