Kamanda wa Polisi Mkoa wa Rukwa, ACP Jacob Mwaruanda
NA MWANDISHI WETU, SUMBAWANGA
CHARLES Kombe (28) mkazi wa Sumbawanga Asilia katika Manispaa ya
Sumbawanga mkoani Rukwa na amekutwa amechinjwa pamoja na majeraha kichwani huku wauaji wakishindwa kuchukua chochote ikiwemo pikipiki yake iliyokutwa imeegeshwa eneo la
tukio.
Tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia leo Jumapili Aprili 19, 2015 katika eneo
la Uwanja wa Ndege mjini Sumbawanga.
Mwili wa marehemu uligunduliwa na watu waliokuwa wakipita njia katika uwanja huo wa ndege ambao waliukuta mwili huo ukiwa umelala
kwenye majani huku pikipiki aliyokuwa nayo marehemu ikiwa imeegeshwa pembeni
yake.
Mashuhuda walimeimbia www.brotherdanny5.blogspot.com kuwa walipokuwa wakielekea kusali alfajiri ambapo waliukuta mwili wa
Charles ukiwa umelala pembezoni mwa
barabara, pikipiki yake ikiwa imeegeshwa kama vile mtu ameiweka anasubiria kitu
ikiwa imezimwa na funguo yake ikiwa imechomekwa kwenye sehemu yake.
Wamesema walipokagua eneo hilo walibaini damu sehemu za kichwani
na simu yake ikiwa kwenye mfuko wa suruali ndipo wakapiga simu
polisi kuwajulisha tukio hilo
ambapo polisi walifika na kuichukua maiti kwa ajili ya kuifanyia
uchunguzi na kuihifadhi katika Hospitali ya Mkoa wa Rukwa, mjini Sumbawanga.
Baba mdogo wa marehemu, Herman Kombe, amesema marehemu alikuwa hanywi pombe enzi za uhai wake na
hakuwa na makundi ya mitaani zaidi ya kazi zake na kusali kila siku ambapo
alikuwa mwanamaombi wa kikundi cha Charismatic cha Kanisa Katoliki.
Amesema enzi za uhai wake marehemu alikuwa akifanya kazi ya
fundi redio katika kibanda kilichopo katika jengo la Ofisi ya CCM Wilaya ya Sumbawanga Mjini,kazi iliyomuweka
karibu na wateja wengi ambao walimuamini.
Amesema jana Jumamosi kabla ya mauti kumfika alizungumza na
marehemu wamtume mtu nyumbani kwao katika Kijiji cha Kirando wilayani humo kupeleka mahitaji ya familia kwa
ajili ya kumalizia msiba wa dada yao aliyefariki katikati ya wiki iliyopita kwa
kutumia pikipiki ya marehemu.
Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Rukwa, Jacob Mwaruanda
alipozungumza na www.brotherdanny5.blogspot.com kwa njia ya simu alikiri kupata
taarifa za kifo na kueleza kuwa yeye na timu yake wanaifanyia kazi taarifa ili
kuwasaka wauaji na kuwatia nguvuni ili waweze kuchukuliwa hatua stahiki kwa
mujibu wa sheria za nchi.
“Tunaendelea na upelelezi wa kina ili kubaini waliofanya uhalifu
huo kwa sababu mpaka sasa hatujapata taarifa sahihi ni nani aliyeshiriki kwenye
kitendo hiki, tunaendelea na kazi tukikamilisha tutawapa taarifa na wala
hatujakamata mtu yeyote mpaka sasa,” amesema.
No comments:
Post a Comment