Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Sunday 19 April 2015

SIMBA YANYOLEWA SHARUBU MBEYA


NA SANULA ATHANAS
Harakati za Simba kuwa moja ya timu mbili zenye uwakilishi wa kimataifa mwakani zilikwaa kisiki nyumbani kwa Mbeya City jana, baada ya kufungwa 2-0 kwenye Uwnja wa Sokoine.


Kwa kipigo hicho, Simba iliyokuwa inawania kuivuka Azam katika nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi kuu ya Bara, inabaki na pointi 35 baada ya mechi 22.

City ina pointi 28 katika msimamo ambao Yanga (46) inaendelea kubaki kileleni licha ya kuwa na kibarua cha kimataifa jana.

City ilijihakikishia ushindi wa mechi hiyo dakika 21 kabla ya filimbi ya mwisho baada ya Peter Mwakianzi aliyeingia kutoka benchini kuwafungasha tela mabeki Juuko Murshid na Isihaka Hassan wa Simba kabla ya kufyatua shuti kali kutoka ndani ya eneo la hatari.

Bao la kwanza la City lilifungwa na Paul Nonga muda mfupi kabla ya mapumziko, akimalizia pasi ya Deus Kiseke kutoka wingi ya kulia kusini mwa Uwanja wa Sokoine, licha ya Peter Manyika kufanya kazi ya ziada kujaribu kuzuia mpira huo.

Nafasi nzuri zaidi kwa Simba kupata japo bao la kufutia machozi ilipotezwa na Awadhi Juma mwishoni kabisa mwa mchezo baada ya kupiga mpira nje akiwa ndani ya mita sita kutoka goli la wenyeji.

CITY: Hannington Kalyesabula, John Kabanda, Hassan Mwasapili, Christian Sembuli, Juma Nyosso, Kenny Alyy, Peter Mapunda (Hamad Kibopile dk.81, Raphael Daud, Paul Nonga, Cosmas Fredy (Peter Mwakianzi dk.49), Deus Kiseke (Selemani Hassan dk.85).

SIMBA: Peter Manyika, Nassoro Cholo, Mohammed Hussein, Hassan Isihaka, Juuko Murshid, Jonas Mkude, Ramadhani Singano, Abdi Banda (Awadh Juma dk.62), Said Ndemla, Ibrahim Ajibu, Elias Maguli.
CHANZO: NIPASHE JUMAPILI

No comments:

Post a Comment