Wahamiaji wakiokolewa baharini
Uchunguzi wa BBC nchini Libya umebainisha mtandao mpana unaotumiwa na walanguzi wanaopata mamillioni ya dolla kupitia usafirishaji wa watu kinyume cha sheria.
Mtu mmoja anaehusika na biashara hiyo amesema kuwa wingi wa watu waliotaka kusafirishwa kwa njia hizo za panya na za hatari umewafanya kuongeza malipo wanayowatoza wahamiaji hao kwa 400%.
Mtu huyo amekiri kuwa boti ndogo wanazotumia ni hafifu lakini hujazwa watu ambao tayari wamewalipa si chini ya dolla 450 kila mmoja, kwa safari hiyo ya kubahatisha ambayo ni dhahiri wengi wao huenda wakapoteza maisha yao.
Mwandishi wetu wa BBC aliyefanya uchunguzi huo anakadiria biashara hiyo kuwa ya thamani ya dolla millioni mia moja na hamsini kila mwaka.
Hivyo ni dhahiri kuwa kundi la wahalifu hao linajitajirisha, na kuwasabishia wengi maafa ya kufa maji na mengineyo , lakini kwa sababu ya ghasia , vita na kuporomoka kwa utawala wa Libya hamna yeyote anaewadhibiti wala kuwawajibisha wahalifu hao.
CREDIT: BBC
No comments:
Post a Comment