Aliyasema hayo kwenye kongamano la uchangiaji wa damu salama lililoandaliwa na kituo cha CG Radio Fm katika maeneo ya sanamu ya mwalimu nyerere mkoani Tabora.
Kumchaya alisema kuwa kuchangia damu salama ni muhimu inamgusa kila mtu ni vema kila mmoja wao ajue anaguswa na kuchangia damu nikujijengea hazina kubwa kwa ndugu zao na kwa jamii kwa ujumla.
Kumchaya ametoa pongezi za dhati kwa kituo hicho cha CG Radio Fm na Benki ya damu kwa kutambua umuhimu wa jambo hilo, Ikiwa ni pamoja na kuwahamasisha wananchi kushiriki katika vzoezi la uchangiaji damu salama.
Kwa upamde wa Meneja Radio na masoko Archard Geogfrey Akisoma risala ,alisema wananchi watambue umuhimu wa kuboresha afya zao ,CG FM Radio kwa kushirikiana na benki ya damu salama kanda ya magharibi wameandaa siku hiyo muhimi ,ili kuhamasisha uchangiaji damu salama kwa lengo la kuwasaidia wananchi.
Geogfey alisema kuwa kazi ya kituo hicho ni kuelimisha jamii na kuburudisha,ili kufanya vizuri ni lazima jamii iwe na afya nzuri na ndio maana wakaona kuhamasisha uchangiaji wa damu salama.
Meneja huyo alisema kuwa wamegundua sekta ya afya ni nyenzo muhimu katika ustawi wa jamii na hususan kwa wasikilizaji wao na waliamua kushirikisha benki ya damu salama kanda ya magharibi ili kuhamasisha wananchi kuchangia damu.
No comments:
Post a Comment