Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Tuesday, 7 April 2015

FANYENI IBADA KULIOMBEA TAIFA-MCHUNGAJI


Na Hastin LiumbaTaboraViongozi wa siasa na serikali wametakiwa kufanya Ibaada za kumuomba Mungu ili kulikomboa Taifa katika  wimbi  la Vitisho vya makundi ya kigaidi.



Akizungumza katika Ibaada ya  sikukuu ya Pasaka Mchungaji Samwel Mmassy wa kanisa la T A G wilayani Nzega Mkoani Tabora alisema Viongozi wengi wamekuwa hawafanyi Ibaada za kweli za kumuomba Mungu badala yake hufanya ibada za uongo.

Alisema Taifa limekuwa likikabiliwa na vitisho vya  kigaidi katika makundi mbalimbali likiwepo la Allshaabab  ambalo limekuwa likifanya mauaji kwa watu  wasio na hatia na kuongeza Taifa na viongozi wafanye Ibada za kweli.

Akizungumzaia katika Nyanja za kiuchumi mchungaji Samweli alisema Taifa linakabiliwa na changamoto za kiuchumi huku baadhi ya wafanyabiashara wakilalamika kushuka kwa uchumi.

Kwa upande wake mchungaji Andrew  Kayamba alisema wananchi wanapaswa kuwaepuka viongozi wanaotoa Rushwa ili kupata viongozi badala yake waangalie viongozi wanaofuata maadili yanayo mpendeza Mungu.

Alisema Taifa lipo katika hatua ya Uchaguzi hivya watanzania wanapaswa kuwaepuka  wagombea wanaoeneza udini,ukabilia  na ukanda badala yake wachague viongozi watakao jali usawa na haki.

Baadhi ya waumini wa kanisa hilo kwa nyakati tofauti walisema kuwa Taifa linapaswa kumrudia Mungu katika kutekeleza yale yaliyo andikwa ilikukabiliana na chaqngamoto zinazojitokeza.

No comments:

Post a Comment