Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Sunday 21 September 2014

WIZARA YA AFYA YASHINDWA KUTIMIZA AHADI YAKE HOSPITALI TEULE YA TUMBI KIBAHA


Katibu mkuu pia anahimiza wananchi kushiriki katika shughuli za maendeleo na kuimarisha chama, Katika msafara huo Kinana anaogozana na Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi, Siasa na Uenezi. Kero kubwa iliyojitokeza katika ziara hiyo ni pale Mkurugenzi wa huduma za Afya katika hospitali ya Tumbi Dr. Peter Dattan aliposema Wizara ya Afya na Ustawi wa jamii iliahidi kununua vifaa vya chumba cha wagonjwa mahututi katika hospitali hiyo(ICU) Lakini ahadi hiyo haijatekelezwa yapata miaka mitatu sasa, Pamoja na kwamba hospitali ya Tumbi Kibaha inapokea majeruhi wengi na wanahitaji tiba maalum kutokana na majeraha mbalimbali yanayosababishwa na majeruhi wa  na ajali, Hospitali ya teule ya Tumbi inapokea asilimia 80% ya majeruhi wa ajali. (PICHA NA KIKOSIKAZI CHA FULLSHANGWE-KIBAHA)
2Mbunge wa jimbo la Kibaha mjini Mh. Silvestry Koka akitoa maelezo ya ujenzi wa ofisi ya CCM wilaya ya Kibaha kwa kwa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana.3Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akifunua kitambaa kama ishara ya kuweka jiwe la msingi katika ujenzi wa ofisi ya CCM wilaya ya Kibaha.4Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki ujenzi wa ofisi ya CCM wilaya ya Kibaha. Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipanda mti katika eneo ambali ofisi ya CCM wilaya ya Kibaha inajegwa mjini Kibaha6Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi, Siasa na Uenezi akipanda mti katika jengo la ofisi mpya ya CCM wilaya ya Kibaha inayojengwa.7Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwapongeza watoto wa chipukizi baada ya kuimba ngonjera yao mbele yake.8Baadhi ya vijana wa Kambi ya vijana ya UVCCM ya wilaya ya Kibaha wakiimba nyimbo kumkaribisha Katibu mkuu Abdulrahman Kinana wakati alipotembelea kambi yao iliyopo Boko Timiza mjini Kibaha.13Katibu Mkuu wa CCM  Ndugu Abdulrahman Kinana akiongozwa na Dr. Peter Dattan Mkurugenzi wa Shughuliza Afya katika hospitali teule ya Tumbi Kibaha, kushoto ni Nape Nnauye Katibu wa NEC Siasa, Itikadi na Uenezi.16Katibu Mkuu wa CCM  Ndugu Abdulrahman Kinana akipata maelezo kutokwa kwa  Dr. Peter Dattan Mkurugenzi wa Shughuliza Afya katika hospitali teule ya Tumbi Kibaha wakati alipotembelea chumba cha wagonjwa mahututi ICU katika hospitali hiyo.17Katibu Mkuu wa CCM  Ndugu Abdulrahman Kinana akipata maelezo kutoka kwa  Dr. Brayson Kiwele  daktari bingwa wa mifupa  katika hospitali teule ya Tumbi Kibaha alipotembelea chumba cha upasuaji.18Katibu Mkuu wa CCM  Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na wafanyakazi wa Mfuko wa Bima ya Afya wa Taifa NHIF mara baada ya kutembelea katika Hospitali Teule ya Tumbi.19Katibu Mkuu wa CCM  Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki kupiga lipu katika ukuta wa tanki la mradi wa maji wa mtaa wa  Muheza mjini Kibaha. 20Katibu Mkuu wa CCM  Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na wananchi wa mtaa wa Muheza mara baada ya kuweka jiwe la msingi katika ujenzi wa mradi huo, aliyesimama juu ni Grace Lyimo Mhandisi wa maji wa wilaya ya Kibaha.21Katibu Mkuu wa CCM  Ndugu Abdulrahman Kinana akiakiwa ofisini kwa Mkuu wa mkoa wa Pwani Mh. Mwantumu Mahiza kulia na kushoto ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Pwani Ndugu Mwinshehe Mlao.22Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mh. Mwantumu Mahiza kushoto akiwa  na baadhi ya viongozi wa CCM mkoa wa Pwani  katikati ni Imani Madega Mlezi wa CCM Mkoa wa Pwani.23Mbunge wa jimbo la Kibaha mjini Mh. Silvestry Koka wakionyesha vyeti vyao baada ya kutambuliwa na uongozi wa CCM mkoa wa Pwani kwa mchango wao wanaoutoa kwa CCM Pwani.

No comments:

Post a Comment