Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Thursday 4 September 2014

VIONGOZI ZAIDI WA UAMSHO WAONGEZWA KESI YA UGAIDI


Idadi ya washtakiwa wanaokabiliwa na kesi ya kula njama na kuwasaidia watendaji wa makosa ya ugaidi kuwaingiza nchini imeongezeka na kufikia 22.

Ni baada ya  wengine wawili, Mselem Mselem na Abdallah Ally kuunganishwa katika kesi hiyo jana.

Mbali na washtakiwa hao wengine ni Kiongozi wa kikundi cha Uamsho na mshtakiwa wa kwanza, Sheikh Farid Hadi Ahmed, Jamal Swalehe, Nassor Abdallah, Hassan Suleimani, Anthari Ahmed, Mohamed Yusuph, Abdallah Hassan maarufu kama Jibaba, Hussein Ally, Juma Juma, Said Ally, Hamis Salum, Said Salum, Abubakar Mngodo, Salum Salum, Salum Amour, Alawi Amir, Rashid Nyange ama Mapala, Amir Juma, Kassim Nassoro na Said Sharifu.

Wakili wa Serikali,  Peter Njike alidai mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Hellen Riwa kwamba upande wa Jamhuri unaomba kubadilisha hati ya mashitaka kwa kuwaunganisha washtakiwa wengine . Hakimu Riwa alikubali ombi hilo.

Njike alidai kuwa  kati ya Januari mwaka 2013 na Juni mwaka huu, washtakiwa hao wanadaiwa kula njama, kuwahifadhi na kuwasaidia watendaji wa makosa ya ugaidi sehemu mbalimbali Tanzania, kinyume na sheria ya kuzuia ugaidi ya mwaka 2002.

Alidai kuwa  katika tarehe tofauti kati ya Januari mwaka 2013 na Juni, mwaka huu katika sehemu mbalimbali Tanzania, washtakiwa hao  walikula njama ya kutenda kosa kinyume na sheria ya kuzuia ugaidi ya mwaka 2002. Katika shitaka la pili, Barasa alidai kuwa siku na tarehe ya tukio la kwanza, washtakiwa wote kwa pamoja, walikubaliana kuwaingiza na kuwasaidia Sadick Absoloum na Farah Omary kutenda kosa la ugaidi sehemu mbalimbali nchini.

Shtaka la tatu, ilidaiwa kuwa siku ya tukio,  mshtakiwa Farid huku akijua na kwa makusudi aliwaingiza na kuwasaidia Sadick na Omary kwa nia ya kutenda kosa la ugaidi sehemu mbalimbali nchini.

Katika shtaka la nne, ilidaiwa kuwa mshtakiwa Farid, huku akijua kwamba wametenda kosa la ugaidi, kwa  makusudi aliwahifadhi Sadick na Omary.

Awali, Hakimu Riwa alisema kwa kuwa mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi za ugaidi, washtakiwa hawatatakiwa kujibu chochote hadi upelelezi utakapokamilika kesi hiyo kuhamishiwa Mahakama Kuu Tanzania, Kanda ya Dar es Salaam.
CHANZO: NIPASHE     

No comments:

Post a Comment