Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Monday 22 September 2014

SERENGETI FIESTA YAPAGAWISHA MASHABIKI MOROGORO


Tamasha la kila mwaka la Serengeti Fiesta, limepagawisha maelfu ya wakazi wa mji wa Morogoro na kuacha simulizi kubwa na  ya aina yake katika mji huo.
Baadhi ya wasanii waliofunika vilivyo katika tamasha hilo na kukonga nyoyo za mashabiki ni pamoja na Mr. Blue, Makomando, Ommy Dimpoz na Stamina.
Stamina ambaye ni mzaliwa wa morogoro alimpandisha mwanamuziki mwingine nguli katika miondoko ya muziki wa kizazi kipya Fid Q bila kutarajia na kufanya mashabiki waliofurika uwanjani hapo kupagawa kwa furaha.
Shoo ilianza taratibu na kadri muda ulivyokwenda ndivyo mashabiki walivyozidi kupagawa. Wasanii hao walikonga nyoyo za mashabiki wao vilivyo na kufanya uwanja wa Jamhuri Morogoro kugubikwa na shangwe kila wakati.
Stamina pia alipanda jukwani na Ney wa Mitego kutumbuiza kwa pamoja kibao chao maarufu kwa jina la “Huko kwenu vipi”.  Mashabiki walisikika wakiimba sambamba na msanii Stamina ambaye ni mzaliwa wa Morogoro.
“Si kila siku shoo zinazofanyika katika viunga vya mji wa Morogoro hupagawisha na kuvuta hisia za watu wengi kama ilivyokuwa wakati wa tamasha la Serengeti Fiesta ,” alisema mmoja wa mashabiki.
Bonanza ya mpira wa miguu na mashindano ya Super nyota Diva yalifanyika kusaka vipaji vya muziki mbali mbali  kutoka  sehemu tofauti  ya mkoa wa Morogoro na washindi walipatikana ambao watasafiri kwenda Dar es Salaam katika shoo ya mwisho.
Wasanii wengine waliopanda katika jukwaa ni pamoja na  Young Killa, Weusi, Afande Sele, Vanessa, Linah, Madee, Mo Music, Baraka Da Prince, Y tony na John Maker.
Primetime Promotions walipata sifa kubwa na kuwa gumzo kwa wakazi wa mji wa Morogoro usiku huo kufuatia utaratibu mzuri waliokuwa wameupanga katika kufanikisha tamasha hilo. 

Akizungumza baada ya shoo, Brand Manager of Serengeti Premium Lager, Rugambo Rodney, alisema…. “Hakika nawashukuru wakazi wa mji wa Morogoro kwa kujitokeza kwa wingi na kuonyesha umoja katika tamasha la Serengeti Fiesta mwaka huu kwani waliweza kushikamana na kusapoti wasanii . Mikoa inayofuatia baada ya hapa ni Mbeya, Mtwara na Songea napenda kuwaambia wakazi wa miji hiyo kuwa wajiandae kujionea shoo nyingine kali kama iliyochezwa hapa Morogoro, ikiletwa kwenu na SBL.

No comments:

Post a Comment