Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Wednesday 13 August 2014

POLISI WAMSAKA MWANACHADEMA ALIYEIBA KADI ZA ACT MBEYA


TAARIFA YAKE KWA UMMA.


KATIKA hali ya kuonyesha ACT ni tishio kwa vyama vingine vya siasa, viongozi wa CHADEMA Mkoani Mbeya wamelazimika kuiba kadi za chama hicho kipya na kuzipeleka ofisini kwao ili ionekane kwamba zimerudishwa kwao na wanachama wa ACT.Tukio hilo lilitokea tarehe 9/8/2014 jijini Mbeya wakati wa sherehe za ufunguzi wa ofisi ya ACT-Tanzania Mkoa wa Mbeya. 

Tukiwa kwenye sherehe za ufunguzi wa ofisi za chama chetu mkoa wa Mbeya, alitokea kada wa CHADEMA Thobias Sebastian ambaye hapo kabla aliwahi kufika katika ofisi za chama chetu kuomba uanachama wa ACT na kukataliwa. Kwa mara ya kwanza alifika ofisini wiki moja iliyopita na kuomba uanachama wa chama, ambapo kamati ya muda ya uongozi wa ACT Mbeya baada ya kujadili maombi yake ya uanachama ikajidhirisha kwamba Thobias hana mwenendo mzuri katika siasa za jijini Mbeya ilimkatalia kumpa uanachama. 

Siku ya sherehe za ufunguzi wa ofisi za chama mkoa wa Mbeya tarehe 10/08/2014, kada huyo wa CHADEMA alionekana akiranda randa kwenye maeneo ya ofisi zetu. Mnamo majira ya saa 11 jioni wakati sherehe imeshika kasi na nje ya ofisi viongozi wa ACT wakiwa wanazungumza na wananchi waliojitokeza kwenye tukio hilo, ghafla tulimwona Thobias akitokea ndani ya ofisi zetu na kuanza kutimua mbio huku akiwa ameshika kadi mpya za ACT mkononi mwake. Viongozi kwa kuhofia kuharibu sherehe waliamua kwenda kuripoti tukio hilo kituo kidogo cha polisi Uyole. Na kwa uzito wa tukio lile na muda ule wa jioni, askari wa zamu alitupa maelekezo viongozi wa ACT kupeleka shauri kituo kikuu cha polisi jijini Mbeya siku itakayofuata. Tumekwisha ripoti kituo kikuu cha polisi na kupaitwa RB NO UY/RB/1815/2014

Pia tumesikitishwa na taarifa za upotoshaji na zisizofuata maadili ya uandishi wa habari kwa kutopata ufafanuzi wa upande wa pili na kupotosha umma wa watanzania zilioandikwa na gazeti la Tanzania Daima la tarehe 11/8/2014. Ni aibu kwa chombo cha habari kuandika habari inayojichanganya, sehemu moja wakisema kadi zilitupwa sehemu nyingine picha ikionyesha anayetuhumiwa kuiba hizo kadi akimkabidhi mbunge wa CHADEMA.

Tunaamini kwa kuwa jambo hili limeripotiwa kwenye vyombo vya usalama jijini Mbeya, sheria itachukua mkondo na vifaa vya ACT vitarudishwa na matendo haya ya kihuni yatakomeshwa kwenye siasa za Tanzania.

KATIBU WA ACT-TANZANIA
MKOA WA MBEYA.

No comments:

Post a Comment