Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Wednesday 20 August 2014

NAWAKUMBUSHA TU: SITTA ALISEMA ANGEIPINGA HOJA YA SERIKALI TATU




Ni vigumu kuelewa kwa nini watu walio tayari kuwabebesha wananchi mzigo wa Serikali Tatu za kudumu, wanahofu gharama za kura ya maoni ya mara moja! Na kama viongozi wetu ni wapumbavu kiasi cha kwamba hawawezi kutunga swali "Je, unataka Serikali Tatu?" Au "Je, unataka Serikali ya Tanganyika?" kazi hiyo wangeweza kuwaachia wataalamu wenye uwezo zaidi. IIa wasiwatukane Watanzania, ambao miaka yote hii wamekuwa wakipiga kura za NDIYO au HAPANA, kwamba ati wakiulizwa swali kama hili watashindwa kulijibu.

Ati kuuliza watu
"Serikali ziwe tatu?"
Ni swali gumu ajabu,
Wanashindwa kulijibu

Tena ati wanasema
Walihofia gharama
Ila serikali tatu

Gharama zake si kitu

Pamoja na hayo, "Taarifa ya SerikaJi inaendelea," kwa kuzingatia kwamba uamuzi wa kura ya maoni ni lazima ukubalike katika sehemu zote mbili za Muungano, itakuwa vigumu kupata uwiano wa kura utakaokubalika, pande rote mbili kuwa ndio kiwango cha uamuzi." Hii ni abracadabra ambayo sielewi kabisa maana yake.

Lakini kwa vyo vyote vile hoja ya kura ya maoni ingeweza kukataliwa, na mambo yakesha. Kwa nini Serikali haikufanya hivyo, ila badala yake ikafufua hoja ya Serikali Tatu?

USUGU WA VIONGOZI:
Jukumu la kueleza taarifa hii ya Serikali katika Halmashauri Kuu ya Taifa aliachiwa Waziri wa Sheria na Mambo ya Katiba, Mheshimiwa Samuel Sitta. Baadaye, baada ya kikao, nilimtafuta Ndugu Sitta, nikampa pole kwa kupewa jukumu la kueleza jambo ambalo halielezeki.

Mapema nilikuwa nimeambiwa kwamba alikuwa ametamka bungeni kwamba hapo hoja ya kudai Selikali Tatu itakapoanza kujadiliwa, yeye ataipinga, maana jimbo lake la uchaguzi, Urambo, halikuwa limemtuma kwenda bungeni kudai Serikali ya Tanganyika. Wabunge wote wakweli wangeweza kusema hivyo hivyo. Hata Waziri Mkuu na Katibu Mkuu wangeweza kusema hivyo hivyo. Wao ni wateuliwa na Rais, ambaye alikwisha kwenda bungeni siku chache tu zilizopita, na kupinga hoja ya Serikali Tatu. Katika kikao cha usiku wa jana yake nilikuwa nimewakumbusha hivyo viongozi wetu waheshimiwa.

Kutokana na mazungumzo yaliyofuatia niliona kuwa bado tulikuwa tunayo nafasi ya kumaliza mgogoro huu bila madhara makubwa. Niliamini kabisa kwamba Serikali ikiondoa mapendekezo yake kukitaka Chama kikubali Serikali Tatu Halmashauri Kuu ya Taifa itairidhika, na wajumbe wake wengi watapumua pumzi za faraja. Na la maana zaidi, nchi yetu itakuwa imeondokewa kwenye ukingo wa shimo la giza. Nilihisi kuwa tatizo ambalo Rais atapata litatokana na washauri wake, maana wao ndio wenye hoja, lakini kwa kuwa yeye ndiye mteuzi wao sikuona kwa nini wawe mgogoro mkubwa. Nilimwambia
hivyo na kuahidi kuwa mimi nitakuwa tayari kumsaidia maeneo yale atakayoona kuwa anahitaji msaada wangu.

Naamini kuwa Rais alijaribu, lakini kama nilivyotazamia washauri wake walikataa. Jitihada na hila za kushawishi wajumbe wa Halmashauri Kuu wakubali Serikali tatu ziliendelea. Hazikufaulu.

Halmashauri Kuu ya Taifa ilikataa kubadili sera yake ya Muungano wenye Serikali mbili; jambo ambalo ndilo lilikuwa shabaha ya viongozi wetu waheshimiwa. Lakini hata hivyo walifaulu kuibabaisha Halmashauri Kuu hata ikakubali kupitisha azimio la kutafuta maoni ya wananchi kuhusu suala la Serikali Tatu. Mimi niliamini kwamba ni kosa.

TENA kusisitiza Muungano wa mbili. Sehemu inayohusika na Azimio la Halamashauri Kuu ya Taifa inasema:

“Chama kifuatilie mjadala wa wananchi Juu ya Azimio hilo na kujipa nafasi ya kujenga mtazamo wake kuunda wa Muungano kabla ya mamuzi ya mwisho. Wakati huu CCM italinda sera yake ya serikali mbili”

Ukizingatia jitihada na hila zilizotumiwa na viongozi wetu kuitaka Halmashauri kuu ikubali hoja ya Serikali Tatu, na pia ukizingatia msimamo wa Kamati Kuu yenyewe, niliona kuwa hata kubaki na sera ya serikali mbli ni ushindi ambao unaweza kutumiwa kuiokoa nchi yetu kutoka katika shimo la maangamizi. Lakini nilitambua kuwa ni hali ngumu sana; mana waheshimiwa hawa walikuwa wametufikisha ambapo Serikali ya Muungano ina sera moja na Chama Cha Mapinduzi kina sera nyingine. Na kwa hila na ujanjajanja wa viongozi wetu wabunge wa Tanzania wamefanywa waonekane kana kwamba katika suala hili, wote kabisa wako upande wa Serikali. Hawa si watu wajinga, wanajua walitendalo.

BUNGE NA CHAMA:

Kabla ya kwenda Dodoma na wakati tukiwa Dodoma, niliambiwa, kwa niaba ya waheshimiwa hao, kwamba Chama Cha Mapinduzi hakiwezi kupinga sera ya Serikali Tatu, maana hiyo ni sera rasmi ya Bunge. Ati Chama hakiwezi kupinga Bunge lake, lakini kwa mantiki ya ajabu ajabu wabunge wanaweza kupinga Chama chao! Hiyo ndiyo demokrasia halisi ya mageuzi. Nilirudi Butiama nikalipa ada yangu ya CCM, na nikaandika utenzi wa Tanzania Tanzania!

Sasa wana hoja nyemi,
Ya kutaka kujihami,
Ni hoja ya kudanganya,
Na kutaka kujiponya

Wanasema viongozi,
Ati Chama hakiwezi,
Kukataa sera hino,
Ya kuvunja Muungano.

Ati serikali mbili,
Sasa ni sera batili;
Maana bunge la watu,
Limetaka ziwe tatu

Chama kisipobadili,
Hiyo ni sera batili,
Kitapinga Bunge lake
Pia Serikali yake.

Na hilo, wanatwambia,
Ni kinyume na kinyume cha sharia,
Siyo halali kwa chama,
Kupinga Bunge la Umma!

Kale twali tukiimba,
Wimbo huu wa kasumba;
Furaha kuu, furaha kuu!
Mikono chini, miguu juu
Twaenda machi, twaenda machi
Twaenda machi, furaha kuu

Hizo ni hoja za wakuu,
Za miguu kuwa juu,
Na vichwa vikawa chini,
Wabunge tahadharini.

Siyo zenu hoja hizi,
Ni hoja za viongozi,
Msizipe uhalali,
Kwani ni hoja batili

Wabunge wa umma,
asili yao ni chama,
wale wa kuchaguliwa,
na walioteuliwa

Sera zao Bungeni,
Zatokana na ilani,
Ya uchaguzi wa nyuma,
Ulofanywa na kauma,
Na wala si sera zao,
Ni sera za chama chao,
Na sababu ya ilani,
Ni kutafuta idhini,
Ya wananchi wenzenu,
Wakubali sera zenu.

Mkishapata kibali,
Mtaunda serikali,
Mtekeleze Bungeni,
Sera zenu, kwa idhini;
Na wale walowatuma,
Ni chama pamwe na Umma.

Ndiyo ma’na na ikasemwa,
Wabunge wakishatumwa,
Wana kauli ya mwisho,
Wasikubali vitisho.

Wameshatumwa na chama,
Kwa idhini ya kauma,
Atowapinga ni nani,
Ila chama pinzani?

Na kwa chama kipinzani,
Kiloshindwa uwanjani,
Kupitisha sera zake,
Kupinga ni haki yake.

Bali kwa ambalo katu,
Hamkutumwa na watu,
Wala si chama chenu,
Ila ni mawazo yenu,
Hamuwezi mkasema,
Kukataliwa na chama,
Si halali, ni haramu,
Na ni kupinga kauma.

Wanaweza viongozi,
Baada ya uchaguzi,
Wakawa wanalo wazo,
Au wana pendekezo,
Wasotumwa na kauma,
Wala si sera ya chama.

Viongozi bila shaka,
Chama chao watataka,
Kijadili jambo hili,
Kipate kulikubali.

Likifanywa sera yao,
Kwa uchaguzi ujao,
Wataandika Ilani,
Waliombee idhini.

Endapo wapiga kura,
Wataikubali sera,
Ndipo tena Bunge lao,
La umma na Chama chao,
Litakwenda kutimiza,
Sera waliyoiagiza.

Serikali haiwezi,
Kwa hila za viongozi,
Ikapitisha Bungeni,
Sera iso na idhini,
Ya chama wala ya umma,
Kisha ianze kusema,
Chama kikichachamaa,
Sera kikaikataa,
Ati hiyo ni haramu,
Chama cha kupinga kaumu

Ni nani alowatuma
Kwa uchaguzi wa nyuma,
Jambo hili ni lao tu,
hawakutumwa na watu.
Kama wanalo haraka,
Kusubiri wamechoka,
Basi wasiwe ajizi,
Waitishe uchaguzi,
Ufanywe hata mwakani,
Waliombee idhini.

Wanasema linapendwa,
Hawawezi kushindwa,
Wanachohofu ni nini,
Kuliombea idhini?

No comments:

Post a Comment