Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Tuesday 19 August 2014

NAWAKUMBUSHA TU: CCM YAIAGIZA SERIKALI KUIPINGA HOJA YA MUUNGANO BUNGENI


Rais mstaafu wa Awamu ya Pili, Alhaj Ali Hassan Mwinyi


Hatua za Serikali baada ya aazimio na mapendekezo

14. Kutokana na Azimio la Bunge, Serikali ya Jamhuri ya Muungano imeona kwamba suala la muundo wa Muungano sasa linahitaji kufanyiwa kazi na kupatiwa uamuzi haraka zaidi na hivyo ni muhimu kuwasilishwa kwenye Chama mapema kwa maelekezo, bila kusubiri mapendekezo ya Kamati ya pamoja ili kuondoa hisia kwamba Serikali inajaribu kulikwepa suala hili.

15. Katika hali hii, Serikali inapendekeza kwamba Halmashauri Kuu ya Chama iafiki pendekezo la Serikali la kuandaa Waraka wa Serikali wa kutafuta maoni ya wananchi (White Paper) kuhusu muundo muafaka wa Muungano kwa kuzingatia mambo yafuatayo:­
(a) Dhana ya kuwa na Serikali tatu ndani ya Muungano, yaani Serikali ya Muungano, Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Serikali ya Tanganyika ikubalike. Muungano wa aina hii kwa Sheria za Katiba na za Kimataifa ni wa Shirikisho (Federa­tion).
(b) Kwamba muundo uwe ni Muungano wenye Serikali tatu, yaani Serikali ya Muungano, Serikali ya Tan­ganyika na Serikali ya Mapinduzi Zan­zibar. Ikumbukwe kwamba neno Muungano linavyofahamika kwenye Sheria za Katiba na za Kimataifa linamaanisha kwamba majukumu yale ya msingi ya dola yanahamishiwa kwenye Serikali ya Muungano."

Haya ni maelezo ya ajabu sana kutoka kwa watu wazima kwenda kwa watu wazima wengine. "Kwanza kabisa", Serikali yetu inaiambia Halmashauri Kuu ya Taifa, "inaonekana kuwa hoja ya awali ingekuwa vigumu kuitekeleza kutokana na muda uliowekwa kufikia Februari, 1994, na pia haikutoa fursa ya kupata maelekezo ya Chama wala Serikali zetu mbili kushauriana.

Aidha, "Kwa kutambua kwamba Bunge linafanya maamuzi yake kwa njia ya kura baada ya mijadala ya wazi wazi, Serikali iliona kwamba hoja yo yote kati ya hizi ingewasilishwa bungeni ingeweza kuligawa Bunge, kukigawa chama chetu na kuwagawa wananchi katika suala zito kama hili la Muundo wa Muungano."

Kwanza, hii "hoja ya awali" ambayo waheshimiwa hawa wanasema hawakuwa na muda wa kutosha kuitekeleza ni ile ya kutaka Serikali Tatu, ambayo kwanza, ni kinyume na sera ya Chama, pili, walikuwa wameagizwa na Kamati Kuu ya CCM siku chache zilizopita wakaipinge Bungeni.

Tatu, tarehe 12 Agosti, 1993, Selikali yenyewe ilikuwa imeliambia Bunge kwamba ilikuwa inaandaa waraka wa kutafuta maoni ya wananchi kuhusu suala hili;

Na nne, (na pengine kutokana na kauli hii ya Serikali), tarehe 20 Agosti, 1993, wabunge wahusika walikuwa wamekwisha kuondoa hoja yao ya awali, nao wakaleta hoja mpya: ya kuitaka Serikali ifanye referendamu ya kutafuta maoni ya wananchi.

Labda waheshimiwa wabunge nao waliona kuwa hoja hii ya kudai Serikali tatu "ikiwasilishwa Bungeni, ingeweza kuligawa Bunge, kukigawa Chama chetu; na kuwagawa wananchi katika suala zito kama hili la Muundo wa Muungano." Mimi siamini hivyo; naamini kuwa kama ingewasilishwa bungeni ili ijadiliwe, ingejadiliwa ikakataliwa na mambo yakesha.­ Maamuzi yoyote ya kidemokrasia hayana budi yatokane na mjadala. Bila ya mjadala, maamuzi, hata yaliyo muhimu kabisa, yatafanywa kwa nguvu hila. Lakini kwa vyo vyote vile, hoja hii, Wabunge wahusika walikwisha kuiondoa.

Kama viongozi wetu waliamini kuwa kujadiliwa kwake kutaleta mgawanyiko huo waliouhofu, kwa nini, basi, walitaka kuitekeleza ila muda wa Wakati CCM ilipotaka kubadili sera yake itatafuta kwanza maoni ya wananchi? Halmashauri Kuu ya Taifa iliketi Unguja ikabadili Azimio la Arusha bila kwanza kutafuta maoni ya wananchi. Na walikuwa na haki kufanya hivyo, maana sera ni yao. Ubaya wao ni kwamba jambo lenyewe walilifanya kwa hila na 'janja janja", na mpaka sasa wanaendelea kudanganya wananchi kwamba sera ya CCM bado ni Ujamaa na Kujitegemea.

Ndivyo viongozi wetu waheshimiwa wanavyojaribu kufanya hata katika suala hili la Muungano. Wanataka kuvunja Tanzania maana "wamechoka na Wazanzibari"; lakini hawataki kusema hivyo wazi wazi. Wanachosema ni kwamba wanataka Serikali ya Tanganyika "ndani ya Muungano", ingawa wanafahamu, maana si watu wapumbavu, kwamba ukifufua Tanganyika utaua Tanzania.

Muundo wa Muungano, pamoja na kwamba hatutaki uwe ukitibuliwatibuliwa mara kwa mara, ni suala la sera, si amri ya Mungu. Vyama vya siasa mbalimbali vinaweza vikawa na maoni mbalinbali kuhusu muundo unaofaa kwa Katiba ya nchi yetu. Muundo utakaokubaliwa na wananchi walio wengi ndio utakaokuwa sehemu ­ya Katiba ya nchi yetu. Muundo wa Serikali mbili unakubaliwa na wananchi, lakini unatokana na sera ya TANU na ASP, na kwa sasa CCM. Chama Cha Mapinduzi kikipenda kinaweza kubadili sera hiyo ya muundo wa Serikali mbili bila kuuliza wananchi kwanza. Kinaweza kufunyahivyo kwa kuhisi kuwa hivyo ndivyo wananchi wengi watakavyo; lakini pia kinaweza kufanya hivyo kwa sababu kinaamini kuwa inafaa kufanya hivyo, hata kama wananchi wengi hawakudai au hawapendi mabadiliko.

Pendekezo hili la kutaka Serikali ya Tanganyika lilizushwa kwanza na Tume ya Nyalali, bila madai ya wananchi. Chama Cha Mapinduzi kikalikataa, kwa sababu nzuri kabisa; lakini kingeweza kulikubali, kama kilivyokubali kuacha mfumo wa chama kimoja na kuleta mfumo wa vyama vingi, pamoja na kwamba wananchi walio wengi walipenda tuendelee na mfumo wa chama kimoja. Maoni ya wananchi yanaweza kukifanya chama kibadili sera zake; lakini si lazima. Chama cho chote kinaweza kubadili sera zake bila kutafuta kwanza maoni ya wananchi. Siku ya Uchaguzi Mkuu maoni ya wananchi yatajulikana.

Nasema, niliamini kuwa ni kosa kwa Halmashauri Kuu ya Taifa kukubali chama kiulize wananchi kama inafaa tuwe na Serikali Tatu. Kwanza, kwa sababu hiyo niliyoeleza; na pili, hata kama CCM ingependa kubadili sera yake, kwa nini turukie Serikali Tatu? Kwa nini tusitake maoni ya wananchi kuhusu Serikali Moja! Au hata kuhusu Serikali za Majimbo? Tumejadili katika vikao gani tukakubaliana kuwa miundo mingine yote haifai, ila muundo unaofaa ni ule wa Serikali Tatu? Au hata Bunge lenyewe, limejadili miundo mbali mbali ya Muungano katika kikao gani, hata wabunge waheshimiwa, pamoja na waheshimiwa mawaziri weiu, wakafikia uamuzi, baada ya mjadala, kwamba muundo peke yake unaofaa ni huu wanaopendekeza, wa kuwa na Serikali Tatu?

Hizi zote ni mbinu za viongozi wetu waheshimiwa kutaka kukiingiza Chama katika njia moja tu nyembamba, na kutuburura kama vipofu tuitumbukize nchi yetu shimoni. Ni jitihada za kukifanya chama, na sisi wengine wote , tuukubali msimamo wao wa kutaka kuigawa nchi yetu.

Lakini kwa bahati njema, pamoja na viongozi wetu, Halmashauri Kuu ya Taifa katika uamuzi wake wa kikao hicho ilirudia kufanya hivyo ndiyo iliokuwa hauwatoshi? Na kwa nini waliifufua tena? Hivi wao waliamini kuwa mjadala wa hoja hiyo- ndio utaweza kugawa Bunge, na Chama na wananchi, lakini kutekelezwa kwake hakutakuwa na matokeo hayo? Na ni nani alikuwa amewatuma wakaitekeJeze?

Pili, Chama ambacho walikuwa hawakupata fursa ya kupata maelekezo yake kuhusu hoja ya Serikali Tatu mpaka sasa sikijui! Chama Cha Mapinduzi kilikwisha kutoa, maelezo yake zamani sana, kilipolikataa pendekezo la Tume ya Jaji Nyalali; Waziri Mkuu alikuwa amelieleza hivyo Bunge kwa maelezo mazuri sana; na Kamati Kuu ilikuwa imeyarudia siku chache tu kabla ya Serikali haijaamua kuipitisha hoja hiyo Bungeni. Selikali ilitaka maelekezo ya Chama gani? Na Serikali zetu mbili zilitakiwa zishauriane kuhusu nini?

Serikali zote mbili ni za Chama Cha Mapinduzi. Na viongozi wake wote ni Wajumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa, ambayo tarehe 10:8: 1993 iliwaagiza wakaipinge hoja ya Serikali Tatu. Walitaka zishauriane juu ya jambo gani?

Hoja ya pili wanayoisema ni ile ya kura ya maoni. Wanasema: "Kuhusu suala la kura ya maoni, Serikali iliona kwamba utekelezaji wake ni sawa na kufanya uchaguzi mkuu, jambo ambalo ni gharama kubwa. Aidha, kwa kuzingatia kuwa kura ya maoni hupigiwa suala linalohitaji jibu NDIYO au HAPANA, ni vigumu kupata swali lililo wazi kwa wananchi ambao hawana uzoefu wa utaratibu huu wa kura ya maoni.


REJEA: NYERERE, J.K.; UONGOZI WETU NA HATMA YA TANZANIA (1994)

No comments:

Post a Comment