Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Monday 25 August 2014

BARUA YA WAZI KUTOKA HIZB UT-TAHRIR KWA BALOZI WA UFARANSA NCHINI KUHUSU MAUAJI YA WAISLAMU AFRIKA YA KATI

Barua Ya Wazi Kutoka Hizb Ut-Tahrir  Kwa Balozi Wa Ufaransa Nchini Jordan Kuhusiana Na Mauwaji Ya Waislamu Wa Afrika Ya Kati

Bwana Balozi,
Uhalifu wa Mauwaji ya Halaiki kwa Waislamu wa Afrika ya Kati unaotendwa na magenge ya wanamgambo wa kikiristo nchini humo unatokana na mipango, kubaki kimya na uratibu wa serikali ya nchi yako. Ufaransa inaunga mkono magenge ya wanamgambo wa kikiristo kwa silaha na inawapendelea waziwazi jamii ya kikiristo nchini humo. Huku nchi yako ikiibuwa na kuchochea chuki zake za kihistoria dhidi ya Uislamu na Waislamu. Pia kuyatumia mauwaji haya ya Waislamu na umwagaji wa damu yao kuwa ndio kisingizio cha kuendelea kuwapo jeshi la Ufaransa katika nchi hiyo.
Bwana Balozi, Sisi Hizb ut -Tahrir tunaelewa fika juu ya ukimya na kutojali kwa nchi yako katika mauwaji haya ya Waislamu na harakati za kuangamiza kabisa kizazi cha Waislamu katika nchi ya Afrika ya Kati. Na sisi kwa upande wetu  tutaendelea kufedhehi ushirika wenu na magenge hayo ya kikiristo na chuki zenu kubwa zinazoendelea dhidi ya Waislamu. Na kamwe haya hayatosahaulika kwa Umma wa Kiislamu mpaka hapo Umma huu utakaposimamisha dola yake ya Kiislamu ya Khilafah ambayo ipo karibu InshaaAllah. Hapo jeuri na uvamizi wenu vitakabiliwa kwa nguvu zote  kwa msuli wa mfumo wa kiudilifu wa Uislamu.
Hapana shaka Bwana Balozi kuwa sharia za Mola wetu katika vita zinatuwajibisha pasiuliwe vizee, watoto, wanawake na  wala kusikatwe miti. Lakini pia tunafahamu kwa kina  kauli ya Mola wetu katika kitabu chake Aliposema:
وَإِنْ عَاقَبْتُمْ فَعَاقِبُوا بِمِثْلِ مَا عُوقِبْتُمْ بِهِ

Na mkilipiza kisasi basi lipizeni sawa na mlivyoadhibiwa” (TMQ Al-Nahl: 126)
Basi kama unavyojuwa Bwana Balozi kwamba Allah kapanga zamu katika kuleta hali za mabadiliko kwa wanadamu. Na sisi tupo ukingoni kusimamisha Dola ya Kiislamu ya Khilafah InshaaAllah. Dola ambayo muda wake unakaribia mno kuliko wewe, serikali yako, nguvu zote za makafiri na madikteta wote wa ulimwengu wanavyodhani.
Sisi tunasema, serikali yako lazima ikomeshe mara moja maangamizi haya ya halaiki ya Waislamu, mauwaji jumla na harakati zote za kiuadui dhidi ya Waislamu. Jambo hili huenda likawa na tija kwenu kwa siku za kiza na majonzi zinazokuja mbele yenu. Na katika masiku hayo kwa udhati kabisa hamtokuwa na  yoyote wa kuwanusuru.
Kumbukeni kwa makini kwamba katika makarne yaliyopita ni dola ya Kiislamu ya Khilafah ndiyo iliyomuokowa Mfalme wa nchi yenu Francois I alipotekwa nyara.  Na Dola ya Kiislamu ikamrejesha tena Ufaransa na akaendelea kutawala.
Kwa hivyo, kumbukeni kuwa dola ya Khilafah kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu itasimamisha  hukmu ya Allah juu yenu kwa uhalifu na ukatili wenu dhidi ya haki za Waislamu.

وَلَتَعْلَمُنَّ نَبَأَهُ بَعْدَ حِينٍ

Na bila ya shaka mtajuwa khabari zake baada ya muda” (TMQ Saad: 88)

Afisi ya Habari Hizb ut Tahrir Wilayah  ya Jordan
Jumatano, 26 Rabii' Thani 1435 AH        26/02/2014 Miladi         No: 17/35

No comments:

Post a Comment