Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Sunday 10 August 2014

LIBERIA YAZIDIWA NA EBOLA

Wafanyakazi wa utabibu waondosha maiti ya mtu aliyekufa na ebola mjini Monrovia

Waziri wa habari wa Liberia amekiri kuwa jinsi ugonjwa wa ebola unavyotapakaa umezidi nguvu za huduma za afya za nchi.
Lewis Brown ameiambia BBC mfumo wa afya umefikia kikomo lakini alikanusha tuhuma kuwa serikali ilichelewa kuchukua hatua, akisema kuwa wakuu wanafanya wawezalo kukabiliana na janga wasilopata kukumbana nalo.
Shirika la msaada wa matibabu la kimataifa, MSF (Medicins Sans Frontiers), limesema kwamba makisio ya wizara ya afya ya Liberia ni madogo ikilinganishwa na ukweli ulioko nchini.Alisema wananchi wengi bado hawakukubali ukweli halisi kuhusu ebola.
Hapo Jumamosi polisi wa kupambana na fujo walivunja maandamano dhidi ya serikali kwa namna ilivoshughulikia hali hiyo.
Inakisiwa kuwa ebola imeuwa watu karibu 1,000 nchini Liberia, Guinea, Sierra Leone na Nigeria.
BBC/SWAHILI

No comments:

Post a Comment