Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Sunday 10 August 2014

CHEZEA ARSENAL WEWE! WATWAA NGAO YA JAMII KWA KUINYUKA MAN CITY 3-0!


Jack WilshereMabingwa wa Kombe la F.A nchini Uingereza Arsenal leo wameonyesha dalili njema za kutoa nuksi kwenye Ligi Kuu baada ya kuichabanga Manchester City kwa mabao 3-0 katika Uwanja wa Wembley katika kuwania Ngao ya Jamii.
Hili ni taji la pili kwa Arsenal katika kipindi cha siku 85 baada ya kukumbwa na ukame kwa siku 3,283 (takriban miaka 9).
Man City, ambao ni mabingwa wa Ligi Kuu, walishindwa kufurukuta mbele ya vijana wa Arsene Wenger baada ya kutandikwa mabao hayo katika mechi hiyo muhimu ya kukata utepe wa pazi la Ligi Kuu.
Tangu ilipobeba la F.A msimu uliopita, kumekuwepo na ari kubwa pale Emirates msimu huu na haikushangaza wakati walipoonyesha kandanda safi lililowafanya waende mapumziko wakiwa mbele kwamabao 2-0.
Mabao ya Arsenal yalipachikwa kimiani na Sandy Carzola, Aaron Ramsey na Olivier Giroud.
Kocha wa Man City, Manuel Pellegrini, alisema timu yake ilielemewa katika kipindi cha kwanza ndiyo maana Arsenal walipata mabao mawili katika kipindi cha kwanza.
"Tulicheza vizuri kwenye kipindi cha pili, tulipata nafasi za kufunga lakini wenzetu waliitumia vyema nafasi pekee waliyoipata na kuongeza bao," amesema baada ya mchezo huo wa kusisimua.
"Mambo haya yanatokea kabla ya kuanza kwa msimu. Kasi yetu haikuwa ile tuliyoionyesha wakati wa mechi za maandalizi ya msimu lakini nitazungumza na wachezaji na nina uhakika tutakuwa imara Ligi Kuu itakapoanza.
Kwa upande wake, Kocha wa Arsenal, Arsene Wenger, alisema: "Mambo mawili yalikuwa muhimu leo; ushindi na taji, hata kama siyo taji kubwa, na kucheza vizuri na ninafurahi kwa sababu tumecheza vizuri.
"Tumeanza vizuri na timu inaridhisha. Tumecheza tukiwa na imani ambayo nimeipenda - mara ya mwisho tulipokuwa kwenye uwanja huu tulikuwa tumefungwa mabao 2-0 ndani ya dakika 20 lakini leo tumekuwa juu kwa mabao 2-0.
"Hii imedhihirisha kwamba timu inapokuwa imedhamiria tuna nafasi ya kushinda mchezo wa ligi. Tunataka kuingia katika kila mechi kwa imani na ujasiri kama huu."

No comments:

Post a Comment