Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Wednesday 13 August 2014

HONGERA PROFESA KITILA MKUMBO!


Ndugu zangu,
Napenda kuchukua fursa hii kumpongeza ndugu yangu, mwanaharakati na school mate wangu (Pugu Secondary School) Kitila Mkumbo kwa kuwa Profesa.
Tunafahamu kwamba elimu yake ya juu kabisa ni Shahada ya Uzamivu (Ph.D) na kwa hivyo tangu mwaka 2008 alipohitimu shahada hiyo katika Chuo Kikuu cha Southampton chini ya Profesa Roger Ingham katika upande wa Elimu ya Jinsia (Sex Edication), amekuwa akitambulia kama Dk. Kitila Mkumbo, lakini kuanzia sasa atakuwa akitambulika kama Profesa Kitila Mkumbo!
Wasifu wake unaonyesha kwamba Shada ya Kwanza na ya Pili katika Saikolojia alizipata Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, mahali ambako aliwahi kuwa Rais wa Serikali ya Wanafunzi (DARUSO) kati ya mwaka 1998-98.
Siyo nia yangu kunadi wasifu wake, lakini niseme tu kwamba, kufikia hatua ya u-profesa siyo lazima uingie darasani, bali inategemea na kutambua kazi zako ulizozifanya katika kiwango cha juu kitaaluma.
Ninamfahamu Profesa Kitila wakati tukiwa pale Pugu Sekondari, tukipanga foleni Majilis, yeye akiwa PCB nami nikiwa O-Level.
Mwaka 1991, wakati huo wengine tukiwa Vijana wa CCM, tulikuwa pamoja kwenye midahalo mbalimbali ya kukusanya maoni ya kuanzishwa kwa mfumo wa vyama vingi vya Siasa Tanzania kabla ya mfumo wenyewe kuanza rasmi mwaka 1992! Ni hapa ndipo nilipotambua kwamba jamaa alikuwa vizuri katika kujenga hoja na kuzitetea.
Ni mpambanaji huyu, lakini zaidi ni mwalimu ambaye waliopitia kwenye madarasa yake wanamweleza kwamba jamaa ametulia katika taaluma, hasa masomo anayofundisha ya saikolojia.
Hongera sana brother or no profesa!

Daniel Mbega,
Iringa

No comments:

Post a Comment