Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia
Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, Mhandisi Hamad Masauni akizungumza
na Waandishi wa Habari mara baada ya kuzindua Mkakati wa Baraza wa Kukabiliana
na Ajali za Barabarani nchini. Mkakati huo wa miezi Sita ambao unalenga
kukabiliana na ajali umenza mwezi huu Agosti na unatarajiwa kumalizika mwezi
Februari 2017 ambapo tathmini itatolewa. Baadhi ya mambo yaliyolengwa katika
mkakati huo ni pamoja na udhibiti wa madereva walevi na kuendesha kwa uzembe,
udhibiti wa mwendokasi kwa madereva na wamiliki wa magari pamoja na kuanza
utaratibu wa Mfumo Nukta (point system) kwenye leseni za udereva ambapo dereva
akifanya makosa kadhaa atanyang’anywa leseni na kutokuruhusiwa kuendesha gari
tena. Uzinduzi huo umefanyika katika
Ukumbi wa Mikutano wa Wizara, jijini Dar es Salaam. Picha zote na Wizara ya
Mambo ya Ndani ya Nchi.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia
Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, Mhandisi Hamad Masauni akizungumza
na Waandishi wa Habari (hawapo pichani) mara baada ya kuzindua Mkakati wa
Baraza wa Kukabiliana na Ajali za Barabarani nchini. Mkakati huo wa miezi Sita ambao
unalenga kukabiliana na ajali umenza mwezi huu Agosti na unatarajiwa kumalizika
mwezi Februari 2017 ambapo tathmini itatolewa. Kulia ni Mkuu wa Kikosi cha
Usalama Barabarani nchini, ambaye pia ni Katibu Mtendaji wa Baraza hilo, Kamanda
Mohammed Mpinga. Uzinduzi huo umefanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Wizara,
jijini Dar es Salaam. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia
Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, Mhandisi Hamad Masauni akizungumza
na Waandishi wa Habari mara baada ya kuzindua Mkakati wa Baraza wa Kukabiliana
na Ajali za Barabarani nchini. Mkakati huo wa miezi Sita ambao unalenga
kukabiliana na ajali umenza mwezi huu Agosti na unatarajiwa kumalizika mwezi
Februari 2017 ambapo tathmini itatolewa. Kulia meza kuu ni Mkuu wa Kikosi cha
Usalama Barabarani nchini, ambaye pia ni Katibu Mtendaji wa Baraza hilo, Kamanda
Mohammed Mpinga. Uzinduzi huo umefanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Wizara,
jijini Dar es Salaam. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
******************************************************************
No comments:
Post a Comment