Mkurugenzi wa
Shirika la Misaada la Maendeleo la Marekani, USAID, Bi. Sharon Cromer, na
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Servacius Likwelile,
wakitia saini Hati ya makubaliano ya msaada wa Zaidi ya shilingi Bilioni 895,
kwaajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo hapa nchini katika
kipindi cha miaka mitano ijayo kuanzia mwaka wa fedha 2016/2020, Jijini Dar es
salaam.
Mkurugenzi wa
Shirika la Misaada la Maendeleo la Marekani, USAID, Bi. Sharon Cromer
(Kushoto), na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Servacius
Likwelile, wakitia saini Hati ya makubaliano ya msaada wa Zaidi ya shilingi
Bilioni 895, kwaajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo hapa
nchini katika kipindi cha miaka mitano ijayo kuanzia mwaka wa fedha 2016/2020,
Jijini Dar es salaam.
Mkurugenzi wa
Shirika la Misaada la Maendeleo la Marekani, USAID, Bi. Sharon Cromer
(Kushoto), na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Servacius
Likwelile, wakibadilishana Hati za makubaliano ya msaada wa Zaidi ya shilingi
Bilioni 895, kwaajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo hapa
nchini katika kipindi cha miaka mitano ijayo kuanzia mwaka wa fedha 2016/2020,
Jijini Dar es salaam.
Mkurugenzi wa
Shirika la Misaada la Maendeleo la Marekani, USAID, Bi. Sharon Cromer
(Kushoto), na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Servacius
Likwelile, wakiwa wameshika Hati za makubaliano baada ya kukamilika kwa
tukio la utiwaji saini makubaliano ya msaada wa Zaidi ya shilingi Bilioni
895, kwaajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo hapa nchini
katika kipindi cha miaka mitano ijayo kuanzia mwaka wa fedha 2016/2020, Jijini
Dar es salaam.
Kaimu Kamishna wa
Fedha za Nje, Wizara ya Fedha na Mipango, Bi. Mamelta Mutagwaba, wakiteta jambo
na Mkurugenzi wa Shirika la Misaada la Maendeleo la Marekani, USAID, Bi.
Sharon Cromer (Katikati), baada ya kukamilika kwa tukio la utiwaji saini
makubaliano ya msaada wa zaidi ya shilingi Bilioni 895, kwaajili ya
utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo hapa nchini katika kipindi cha
miaka mitano ijayo kuanzia mwaka wa fedha 2016/2020, Jijini Dar es salaam.
Na Benny Mwaipaja, MoFP, Dar es salaam
SERIKALI ya
Marekani, kupitia shirika lake la Misaada ya Maendeleo USAID, imeipatia
Tanzania msaada wa dola Milioni 407 sawa na zaidi ya shilingi Bilioni 895
zitakazotumika kwaajili ya kuendeleza sekta za Kilimo, Afya, Nishati ya Umeme,
Elimu na Utawala Bora, katika kipindi cha miaka mitano ijayo kuanzia mwaka
2016/2020.
Hati za Makubaliano
hayo zimetiwa saini Jijini Dar es salaam, kati ya Mkurugenzi wa Shirika la
USAID, Bi. Sharon Cromer, na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango
Dkt. Servacius Likwelile.
Msaada huo ni
sehemu ya dola Milioni 800, sawa na zaidi ya shilingi Trilion 1.76 ambazo
serikali ya Marekani kupitia USAID, imepanga kuipatia Tanzania ili kufanikisha
Mpango wa Pili wa Maendeleo wa Taifa katika kipindi cha miaka mitano ijayo,
wenye lengo la kuiwezesha Tanzania kufikia uchumi wa kati kupitia sekta ya
viwanda ifikapo mwaka 2025.
Kiasi hicho cha
fedha kitatumika na serikali ya Tanzania kupitia mfuko mkuu moja kwa moja
wakati kiasi kingine kitatumiwa na Taasisi zisizokuwa za kiserikali zinazofanya
shughuli zake hapa nchini kufanikisha malengo ya msaada huo.
Miradi iliyopewa
kipaumbele ni pamoja na kupambana na UKIMWI na Kifua Kikuu, Uzazi wa Mpango,
Kupunguza vifo vya mama na mtoto, kukuza utawala wa kidemokrasia, Usimamizi wa
Rasilimali za Taifa, na kuwekeza kwenye sekta ya umeme ili kuimarisha sekta ya
viwanda na uzalishaji mali.
No comments:
Post a Comment