Na
Mathias Canal, Singida
Ushiriki wa wananchi katika shughuli za maendeleo kwa
kutumia nguvu na akili katika kukamilisha na kumiliki miradi ya kijamii
imetajwa kuwa njia mojawapo itakayowafanya wananchi kuwa na uchungu na mali
pamoja na maendeleo ya katika jamii husika.
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Miraji Jumanne Mtaturu amesema kuwa kumekuwa na matumizi mabaya ya
demokrasia katika Wilaya hiyo hususani katika shughuli za kijamii kama vile
kuchangia ujenzi wa maabara jambo lililopelekea Wilaya hiyo kuwa ya mwisho
katika ujenzi wa maabara kwa ajili ya shule za sekondari zilizopo katika Wilaya
ya Ikungi.
Mtaturu amesema kuwa hakuna demokrasia yoyote duniani
inayohubiri wananchi kutoshiriki shughuli za maendeleo hivyo mwananchi anapaswa
kushirikishwa katika kuchagua viongozi wake, kukaa na viongozi wake kupanga
miradi ya maendeleo kama vile kuchangia ujenzi wa shule, zahanati na maabara.
“Wataalamu wa Sayansi na viongozi mashuhuri wamewahi
kusema Demokrasia bila maendeleo sio demokrasia, Hayati Mwalimu julius Kambarage Nyerere na Profesa Issa Shivji waliwahi
kuandika kuwa demokrasia ya kweli ni ile inayowasaidia wananchi kutoka katika
hali moja kwenda kwenye hali nyingine ambayo ni bora zaidi kuliko ile waliyo
nayo, hivyo tukiongelea kuwashirikisha wananchi katika mipango na mikakati ya
kuondokana na umasiki na si vinginevyo” Alisema
Mtaturu.
Dc
Mtaturu amesema kuwa kuwa
mwenyekiti wa Kijiji kutoka Chama cha Mapinduzi (CCM), CHADEMA, ACT WAZALENDO,
CUF au chama chochote hapaswi kuongoza wananchi kwa matakwa yake binafsi bali
ni lazima kufuata taratibu, kanuni, sheria na taratibu zinazowaongoza katika
kutekeleza majukumu yao.
Ameyasema hayo wakati wa kikao cha kazi kati ya Mkuu
waWilaya Wakuu wa idara na vitengo, Maafisa Tarafa, Weneyeviti wa Vijiji na
Watendaji wa Kata na Vijiji katika mafunzo yaliyofanyika katika ukumbi wa
Halmashauri ya Wilaya hiyo.
Amewaelekeza wenyeviti wa Vijiji kuwa majukumu yao ni kuongoza vikao vya Halmashauri ya
Kijiji na kuongoza mkutano mkuu wa Kijiji sio kuuza ardhi ya kijiji kiholela,
Kumnyang’anya mtu ardhi au kupiga faini yoyote wanayojisikia na ndio maana
kunakuwa na watendaji wa Vijiji ambao ni wataalamu hivyo wana majukumu muhimu
katika kuwashauri wenyeviti wa Vijiji.
Dc
Mtaturu pia amewataka viongozi hao kutambua kuwa uchaguzi
ulimalizika Octoba mwaka jana na chama kilichoshika dola ni Chama Cha Mapinduzi
(CCM) hivyo kutokana na uchaguzi huo Chama Cha Mapinduzi (CCM) kilipewa ridhaa
ya kuongoza Tanzania kwa kipindi cha miaka mitano 2015-2020 hivyo ilani
inayotekelezwa na serikali ya awamu ya Tano ni ilani ya Chama Cha Mapinduzi
(CCM) hivyo kwa vile kila kiongozi wa Kijiji yupo ndani ya serikali anapaswa kutelekeza
ilani ya CCM kwani huo ni utaratibu wa vyama vinavyoshinda popote dunia.
Baadhi ya watendaji wa Kata, Wenyeviti wa Vijiji, na
baadhi ya watendaji wa Vijiji Wilayani Ikungi hawajawahi kupatiwa mafunzo ya
muongozo wa kiutendaji hali iliyopelekea baadhi yao kutotimiza wajibu wao na
wengine kufanya kazi nje ya mipaka yao.
“ Kupitia kikao/mafunzo haya Uonevu wowote, kosa
lolote, matumizi mabaya ya madaraka yatakayofanywa aidha na Mtendaji wa Kata,
Mwenyekiti wa Kijiji, Mtendaji wa Kijiji sitalifumbia macho nitakuchukulia
hatua kwa mujibu wa sheria, kanuni, tulizowekeana kama serikali” Alisema Mtaturu
Sambama na hayo Dc
Mtaturu amewasihi viongozi hao kuwaunga mkono askari polisi katika
kuimarisha ulinzi na usalama kwani bila usalama na amani katika jamii inayotuzunguka
hakuwezi kuwa na maendeleo.
No comments:
Post a Comment