Mkuu wa Fedha na Tahadhari wa Huduma ya Fedha kwa njia ya mtandao wa Kampuni ya simu ya Tigo, Obedi Laiser (kushoto), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, kuhusu gawio la mwaka huu kwa watumiaji wa Tigo Pesa ambalo watumiaji hao wameanza kulipata kuanzia jana. Kulia ni Meneja wa Mawasiliano wa Tigo, John Wanyancha.
Wanahabari wakichukua taarifa hiyo.
Meneja wa Mawasiliano wa Tigo, John Wanyancha (kulia), akizungumza katika mkutano huo.
Na Dotto Mwaibale
Kampuni
inayongoza katika kuleta maisha ya kidijitali kwa jamii, Tigo,
imetangaza tena malipo ya robo mwaka ya shilingi bilioni 4.4 (dola
milioni 2.1) kwa watumiaji wake wa huduma ya Tigo Pesa wapatao milioni
4.6.
“Gawio
hili la faida linalipwa kwa watumiaji wote wa Tigo Pesa wakiwemo wateja
binafsi, mawakala wa rejareja na washirika wetu wa kibiashara, kila
mmoja kutokana na thamani ya fedha aliyojiwekea katika akaunti yake ya
Tigo Pesa,” alisema Mkuu wa Fedha na Tahadhari wa Huduma ya Fedha kwa
njia ya mtandao, Obedi Laiser.
Akizungumza
katika mkutano wa waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Laiser
alisema kuwa hii itakuwa ni mara ya kwanza Tigo kuwalipa gawio la faida
watumiaji wa Tigo Pesa kwa mwaka wa 2016 akibainisha kuwa malipo hayo
ni faida inayopatikana kutokana na amana ya mfuko wa Tigo Pesa
uliyowekezwa katika benki za kibiashara hapa nchini.
“Tunayo
furaha kubwa kutangaza gawio hili la faida kwa mara ya saba mfululizo
tangu tulivyoanza kufanya hivi mwaka 2014. Bila shaka hii inaonyesha ni
jinsi gani Tigo inajizatiti kuwaletea watanzania maisha bora ya malipo
kwa njia ya mtandao,” amesema Laiser.
Tigo ilikuwa kampuni ya kwanza duniani kutoa gawio kwa wateja wake mwaka 2014
“Tunaamini
gawio hili la kwanza la faida ya Tigo Pesa kwa mwaka 2016 litakuwa ni
kivutio kikubwa kwa mamilioni ya watumiaji wa Tigo Pesa katika
kufanikisha mahitaji yao mbalimbali ya kifedha ya mwanzo wa mwaka,”
amesema Laiser.
Malipo
haya kwa watumiaji wa Tigo Pesa hutolewa kwa mujibu wa mwongozo wa
Benki Kuu uliotolewa mnamo Februari mwaka 2014. Mpaka sasa Tigo imelipa
jumla ya bilioni 35.5 kwa wateja wake tangu kuanzishwa kwa utaratibu huu
mwaka juzi na kampuni hiyo.
No comments:
Post a Comment