Naibu
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Balozi Simba Yahya, (kushoto) akisalimiana
na maafisa wa Jeshi la Magereza alipotembelea Gereza la uzalishaji mifugo Mtego
wa Simba lililopo Kingolwira mkoani Morogoro.
Naibu
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Balozi Simba Yahya, akisaini
kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili katika Gereza la uzalishaji mifugo
Mtego wa Simba mkoani Morogoro. Kulia ni Mkuu wa Gereza hilo Mrakibu Mwandamizi
wa Magereza, Omari Msepwa.
Mrakibu
Msaidizi wa Jeshi la Magereza katika shamba la uzalishaji mifugo Gereza la
Mtego wa Simba, Constatus Magori akitoa maelezo kwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara
ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Balozi Simba Yahya (kushoto) alipotembelea Gereza
hilo Januari 30, 2016 kujionea shughuli mbalimbali za uzalishaji zinazofanywa
gerezani hapo mkoani Morogoro.
Kundi
la ng’ombe wa maziwa wanaofugwa katika shamba la uzalishaji mifugo Gereza la
Mtego wa Simba, Kingolwira mkoani Morogoro wakiwa malishoni kama wanavyoonekana
katika picha.
Mtaalamu
wa mifugo katika mradi wa ufugaji kuku wa mayai na nyama uliopo Gereza Kuu la
Wanawake Tanzania, lililopo Kingolwira mkoani Morogoro, Sajenti Sarah Kabunda (wapili
kushoto) akitoa maelezo kwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya
Nchi, Balozi Simba Yahya (kushoto) alipotembelea Gereza hilo Januari 30, 2016 kujionea
shughuli mbalimbali za uzalishaji
zinazofanywa gerezani hapo.
Naibu
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Balozi Simba Yahya (wa pili kushoto),
akiangalia moja ya mashuka yanayofumwa kwa ustadi mkubwa na wafungwa wa kike
katika Gereza Kuu la Wanawake Tanzania, Kingolwira mkoani Morogoro. (Picha na
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi).
No comments:
Post a Comment