Katibu
Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira
(kushoto) akimsalimia Mkuu wa Jeshi la Magereza, Kamishna Jenerali (CGP), John
Minja wakati alipokuwa anawasili ofisi ya Makao Makuu ya Jeshi hilo, jijini Dar
es Salaam leo kwa ajili ya ziara ya kikazi. Katibu Mkuu Rwegasira alilipongeza
jeshi hilo kwa utendaji wa kazi mzuri licha ya kuwa wanakabiliwa na changamoto
mbalimbali. Kulia ni Kamishna wa Fedha na Utawala wa Jeshi hilo, Gaston Sanga,
na anayefuata ni Kamishna wa Sheria na Utawala wa Jeshi hilo, Dk Juma Malewa. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya
Nchi.
Mkuu
wa Jeshi la Magereza, Kamishna Jenerali (CGP), John Minja akitoa taarifa ya
utendaji wa Jeshi lake kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja
Jenerali Projest Rwegasira (katikati meza kuu) wakati Katibu Mkuu huyo
alipofanya ziara ya kikazi Makao Makuu ya Jeshi hilo, jijini Dar es Salaam. Katibu
Mkuu Rwegasira alilipongeza jeshi hilo kwa utendaji wa kazi mzuri licha ya kuwa
wanakabiliwa na changamoto mbalimbali. Kushoto meza kuu ni Naibu Katibu Mkuu wa
Wizara hiyo, Balozi Simba Yahya. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira (katikati)
akizungumza na Makamanda wa Jeshi la Magereza wakiongozwa na Kamishna Jenerali,
John Minja (kushoto meza kuu) wakati Katibu Mkuu na Naibu wake walipofanya
ziara ya kikazi Makao Makuu ya Jeshi hilo, jijini Dar es Salaam leo. Katika
hotuba yake, Meja Jenerali Rwegasira alilipongeza jeshi hilo kwa utendaji wa
kazi mzuri licha ya kuwa wanakabiliwa na changamoto mbalimbali. Kulia ni Naibu
Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Balozi Simba Yahya. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani
ya Nchi.
Naibu
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Balozi Simba Yahya (kulia) akizungumza
na waandishi wa habari mara baada ya kumaliza mazungumzo na Makamanda wa Jeshi
la Magereza wakiongozwa na Kamishna Jenerali, John Minja (wapili kulia) wakati Katibu
Mkuu na Naibu Katibu Mkuu huyo walipofanya ziara ya kikazi ofisi za Makao Makuu
ya Jeshi hilo, jijini Dar es Salaam leo. Katika hotuba yake, Balozi Simba
alilitaka jeshi hilo wawatumie wafungwa wenye makosa madogomadogo kama nguvu
kazi ili waongeze uzalishaji ndani ya jeshi hilo. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Mkuu
wa Jeshi la Magereza, Kamishna Jenerali, John Minja (kushoto) akimkabidhi Katibu
Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira (katikati)
taarifa ya kiutendaji ya Jeshi hilo. Kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo,
Balozi Simba Yahya. Viongozi hao wa Wizara walifanya ziara ya kikazi katika ofisi
ya Makao Makuu ya jeshi hilo, jijini Dar es Salaam leo. Picha zote na Wizara ya Mambo ya
Ndani ya Nchi.
KITENGO CHA
MAWASILIANO YA SERIKALI,
WIZARA YA MAMBO
YA NDANI YA NCHI
No comments:
Post a Comment