Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Nape Nnauye akifungua Mwaka Mpya
Kichina wa 2016 unaojulikana kama mwaka wa “Ngedere” kulingana na utamaduni wa
nchi hiyo mwishoni mwa wiki viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam.
Kushoto ni mshereheshaji ajiyejitambulisha kwa jina la “Sharobaro”.
Waziri
wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Nape Nnauye (kushoto) akibadilishana
mawazo na Waziri Mkuu Mtaafu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Salim
Ahmed Salim (kulia) wakati wa hafla ya uzinduzi wa Mwaka Mpya Kichina wa 2016
unaojulikana kama mwaka wa “Ngedere” kulingana na utamaduni wa nchi hiyo
mwishoni mwa wiki viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Nape Nnauye (kulia) akifuatilia
michezo mbalimbali wakati wa wa hafla ya uzinduzi wa Mwaka Mpya Kichina wa 2016
unaojulikana kama mwaka wa “Ngedere” kulingana na utamaduni wa nchi hiyo
mwishoni mwa wiki viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam. Kushoto ni
Mshauri wa Mambo ya Utamaduni kutoka Ubalozi wa China nchini Tanzania Gao Wei.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Nape Nnauye (katikati) akifuatilia
michezo mbalimbali wakati wa wa hafla ya uzinduzi wa Mwaka Mpya Kichina wa 2016
unaojulikana kama mwaka wa “Ngedere” kulingana na utamaduni wa nchi hiyo
mwishoni mwa wiki viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam. Kulia ni Waziri
Mkuu Mtaafu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Salim Ahmed Salim na
kushoto ni Mshauri wa Mambo ya Utamaduni kutoka Ubalozi wa China nchini
Tanzania Gao Wei.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Nape Nnauye (kushoto) akifuatilia
michezo wakati wa hafla ya uzinduzi wa Mwaka Mpya Kichina wa 2016 unaojulikana
kama mwaka wa “Ngedere” kulingana na utamaduni wa nchi hiyo mwishoni mwa wiki viwanja
vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam. Kulia ni Waziri Mkuu Mtaafu wa Serikali
ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Salim Ahmed Salim.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Nape Nnauye (kushoto) akisalimiana
na Waziri Mkuu Mtaafu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mizengo
Pinda (kulia) alipowasili viwanja vya Mnazi Mmoja wakati wa hafla ya uzinduzi
wa Mwaka Mpya Kichina wa 2016 unaojulikana kama mwaka wa “Ngedere” kulingana na
utamaduni wa nchi hiyo mwishoni mwa wiki viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es
salaam.
Mawaziri Wakuu Wastaafu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Salim
Ahmed Salim (kulia) na Mizengo Pinda (kushoto) wakisalimiana wakati wa hafla ya
uzinduzi wa Mwaka Mpya Kichina wa 2016 unaojulikana kama mwaka wa “Ngedere”
kulingana na utamaduni wa nchi hiyo mwishoni mwa wiki viwanja vya Mnazi Mmoja
jijini Dar es salaam.
Baadhi ya wageni waliohudhuria
hafla ya uzinduzi wa Mwaka Mpya Kichina wa 2016 unaojulikana kama mwaka wa
“Ngedere” kulingana na utamaduni wa nchi hiyo mwishoni mwa wiki viwanja vya
Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam.
Baadhi ya raia wa Kichina
wakiendelea na kujipamba kabla ya kuanza kwa hafla ya uzinduzi wa Mwaka Mpya
Kichina wa 2016 unaojulikana kama mwaka wa “Ngedere” kulingana na utamaduni wa
nchi hiyo mwishoni mwa wiki viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam.
Baadhi ya michezo iliyooneshwa
wakati wa hafla ya uzinduzi wa Mwaka Mpya Kichina wa 2016 unaojulikana kama
mwaka wa “Ngedere” kulingana na utamaduni wa nchi hiyo mwishoni mwa wiki
viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam.
Waziri Mkuu Mtaafu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mizengo Pinda
akichanganya tiketi za bahatinasibu wakati wa hafla ya uzinduzi wa Mwaka Mpya
Kichina wa 2016 unaojulikana kama mwaka wa “Ngedere” kulingana na utamaduni wa
nchi hiyo mwishoni mwa wiki viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam.
Vimulimuli vy fataki zilizowashwa
kuashiria kuzinduliwa kwa Mwaka Mpya Kichina wa 2016 unaojulikana kama mwaka wa
“Ngedere” kulingana na utamaduni wa nchi hiyo mwishoni mwa wiki viwanja vya
Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam.
(Picha
na Eleuteri Mangi-MAELEZO)
Na Eleuteri Mangi-MAELEZO
Jumuiya ya Wachina wanaoishi nchini
wamezindua na kuukaribisha kwa shamrashamra mwaka Mpya wa 2016 unaojulikana
kama mwaka wa “Ngedere” kulingana na utamaduni wa nchi hiyo mwishoni mwa wiki
jijini Dar es salaam.
Akizindua shamrashamra hizo, Waziri wa
Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Nape Nnauye alisema kuwa Wachina na
Watanzania ni ndugu ambao uhusiano wao ni wa kudumishwa milele na milele.
“Uhusiano wa Tanzania na China ni wa
kihistoria ambao ni wa muda mrefu katika mambo mbalimbali ikiwamo kijamii, kiuchumi,
kisiasa, kielimu na kiutamaduni Utamaduni na kimawasiliano kati ya nchi hizi
mbili” alisema Waziri Nape.
Kihistoria, uhusiano wa China na
Tanzania ni wa kidugu na kirafiki wakati wote iwe wa dhiki au faraja katika
maisha ya kila siku kati ya Watanzania na Wachina.
Ni wakati muafaka kuongeza jitihada za
kuimarisha uhusiano na ushirikiano wan chi hizo mbili ili kuwaenzi waasisi wa
ushirikiano huo ambao ni Rais Mwalimu Julius Nyerere na Mao Tse Tung.
Kwa upande wake Mshauri wa Mambo ya
Utamaduni kutoka Ubalozi wa China nchini Tanzania Gao Wei alisema kuwa
wanajisikia faraja wakati wote wanapofanya kazi na Watanzania kwa kuwa
wanamengi ya kujivunia katika historia ya nchi hizo.
Aidha, shamrashamra za mwaka mpya wa
Kichina zilihudhuriwa na wageni mbalimbali wakiwemo Mawaziri Wakuu Wastaafu
Salum Ahmed Salum, Mizengo Pinda, viongozi mbalimbali na wenyeji wa sherehe
hizo ambao ni raia wa Kichina wanaoishi nchini wakiongozwa na viongozi kutoka
Ubalozi wa China nchini Tanzania.
Mwaka huu unajulikana kama “Ngedere”
wakati mwaka 2015 ulijuklikana kama “Kondoo” ambapo maadhimisho ya Mwaka Mpya
wa “Ngedere” yalipambwa na michezo mblimbali ikiwemo bahatinasibu, sarakasi,
nyimbo, muziki wa ala, mazingaombwe na ngoma.
No comments:
Post a Comment