Wananchi
wa Kata ya Usagara, wilayani Misungwi wakimshangilia Waziri wa Mambo ya Ndani
ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Misungwi mkoani Mwanza, Charles
Kitwanga wakati alipokuwa akizungumza na wananchi hao katika Viwanja vya Gulio mjini
Usagara. Wananchi hao walimwambia Waziri Kitwanga wanaikumbuka ahadi ya Rais John
Magufuli wakati akiwa anamnadi Mbunge huyo kipindi cha kampeni, kuwa suala la
maji atalishughulikia Rais mwenyewe. Hivyo wanamuomba Mbunge wao ashirikiane na
Rais huyo ili maji yaweze kupatikana kwa haraka zaidi. Picha zote na Felix Mwagara.
Kikundi
cha Burudani kinachoitwa Mawe Matatu cha Kata ya Usagara, wilayani Misungwi
kikitoa burudani kabla ya Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni
Mbunge wa Jimbo la Misungwi mkoani Mwanza, Charles Kitwanga (kulia-aliyekaa)
kuzungumza na wananchi wa kata hiyo katika Viwanja vya Gulio mjini Usagara. Katika
hotuba yake, Waziri Kitwanga aliwashukuru wananchi hao kwa kumchagua na pia
atahakikisha kero zote anazitatua. Hata hivyo, wananchi hao,walimwambia Waziri
Kitwanga wanaikumbuka ahadi ya Rais John Magufuli wakati akiwa anamnadi Mbunge
huyo kipindi cha kampeni, kuwa suala la maji atalishughulikia Rais mwenyewe.
Hivyo wanamuomba Mbunge wao ashirikiane na Rais huyo ili maji yaweze kupatikana
kwa haraka zaidi.
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Misungwi mkoani
Mwanza, Charles Kitwanga akizungumza na wananchi wa Kata ya Usagara kuhusu
masuala mbalimbali ya maendeleo ya jimbo lake. Kitwanga aliwataka wananchi hao
washirikiane katika kuchangia miradi ya maendeleo ili jimbo hilo liweze kupata
mafanikio zaidi. Hata hivyo, wananchi hao walimuambia Waziri Kitwanga
wanaikumbuka ahadi ya Rais John Magufuli wakati akiwa anamnadi Mbunge huyo
kipindi cha kampeni, alisema suala la maji atalishughulikia Rais mwenyewe, hivyo
wanamuomba Mbunge wao ashirikiane na Rais huyo ili maji yaweze kupatikana kwa
haraka zaidi. Hata hivyo maandalizi ya upatikanaji maji zimeanza jimboni humo.
Msimamizi
wa Mradi wa Maji Mwanza, Abbas Muslim akijibu maswali ya wananchi baada ya Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Misungwi, Charles
Kitwanga (kulia) kumtaka ajibu maswali ya wananchi hao kuhusu lini maji
yatapatikana jimboni humo pamoja na hatua walizozifikia mpaka sasa. Hata hivyo,
Msimamizi huyo alitoa ufafanuazi kuhusu mradi huo na kuwafafanulia wananchi hao
kuwa, mradi huo mkubwa wa maji unaojumuisha Misungwi, Magu, Lamadi, Musoma,
Bukoba na Jiji la Mwanza unatarajiwa kumalizika mwaka 2018 lakini pia unaweza
ukamalizika kabla ya muda huo uliopangwa na wananchi kuweza kupata maji. Picha
zote na Felix Mwagara.
***************************************************************************
No comments:
Post a Comment