January Makamba
NA RAISA SAID, BUMBULI
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais anayeshugulikia Muungano na Mazingira,January Makamba ametoa msada wa mabati 300 kwa wananchi ambao nyumba zao zimeezuliwa na upepo uliosababishwa na mvua kubwa iliyonyesha maeneo mbalimbali jimboni humo.
Nyumba hizo zilikuwa 40 ikiwemo Kanisa na Msikiti zimeezuliwa mapaa katika kijiji cha Msamaka kilichopo wilayani Bumbuli kufuatia Mvua kubwa iliyoambatana na upepo kunyesha.
Mvua hiyo imesabisha kaya hizo kukosa mahali pa kuishi , huku wengi wa waathirika wakipewa hifadhi kwenye nyumba za majirani zao.
Akizungumza na waandishi wa habari hapo Jana Afisa Mtendaji wa kijiji cha Msamaka Mbazi Shemhando alisema kuwa tukio hilo lilitokea mnamo January 27 mwaka huku saa kumi jioni.
Alitaja sehemu zilizo athirika zaidi kuwa ni Vitongoji vya Kwemchaa, Nazareti,CCM, Kwakorosi pamoja na kitongoji cha Kwamingojo ndio vimeweza kuathirika na maafa hayo.
Hata hivyo aliongeza kuwa waathirika watukio hilo Kwa sasa wamehifadhiwa kwenye nyumba za Jirani wakati utaratibu mwingine wa kuwasaidia ukiendelea kuwekwa.
Akikabidhi msaada huo Makamba alisema kuwa kutokana na tukio hilo anatanguliza msaada huo kwanza wakati akiendelea kutafuta msaada zaidi.
"Nimejikusanya Kwa hiki kidogo ili kiweze kusaidia pale penye uhitaji Kwa haraka wakati tukiendelea na utaratibu mwingine" alisema Makamba.
Makamba aliwataka wananchi wote kupanda miti ili kuepuka upepo mkali unaosababishwa na mvua zinazoendelea kunyesha katika maeneo tofauti
No comments:
Post a Comment