Spika wa zamani wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samuel Sitta akiteta jambo na Alex Msama.
Na Mwandishi Wetu
ALIYEKUWA Mwenyekiti wa Bunge la Katiba pendekezwa, Samuel Sitta ametoa wito kwa waandaaji wa Tamasha la Pasaka, Kampuni ya Msama Promotions kutosahau Kwaya za Makanisa mbalimbali.
Kwa mujibu wa Sitta Msama wasiweke mkazo kwa waimbaji pekee bali pia na kwaya za makanisa ambazo mchango wake nao unatambulika.
Sitta anampongeza Alex Msama baada ya tamasha hilo mapato yake yanasaidia makundi yenye uhitaji maalum kama yatima, wajane na walemavu ambao mara nyingi wanawakumbuka.
Sitta alisema matamasha hayo yana malengo mazuri kwa watanzania, hivyo wadau wanatakiwa kumuongezea nguvu katika ufanikishaji wake.
Sitta alisema Kwaya za Katoliki, Lutherani, Assemblies of God na nyinginezo sambamba na Kwaya za nje ili kubadilishana uzoefu kati ya kwaya za Tanzania na nje.
"Miaka ya hivi karibuni, Kwaya za makanisani tumezisahau, tuzitumie kwa sababu nazo ni eneo letu," alisema Sitta.
Naye Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi ya tamasha hilo, Alex Msama alisema wanapokea mawazo ya Sitta ni ya muhimu, hivyo Kamati ya maandalizi wanayafanyia kazi maombi ya wadau mbalimbali ili kuliboresha zaidi.
Msama alisema hivi sasa wanasubiri kupatikana kwa kibali kutoka Baraza la Sanaa la Taifa (Basata) ili kuendelea na taratibu za kufanyika kwa tamasha hilo.
No comments:
Post a Comment