Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Tuesday, 14 April 2015

WANANCHI WACHOMA NYUMBA YA KIKONGWE KWA KUZUIA MVUA.



IGP Ernest Mangu
Na Hastin Liumba, Igunga.
Zaidi ya watu 40 wamemvamia kikongwe na kuchoma nyumba yake  huku wakimcharaza mke wake bakora wakimtuhumu kuzuia kunyesha mvua katika kijiji cha Mwakwangu kata ya Igurubi wilayani Igunga mkoani Tabora.



Akizungumza kwa masikitiko na gazeti hili katika eneo la tukio, mhanga wa tukio hilo Mayala Jinayi (70) alisema yeye na mke wake Sophia Mahona (50) walikuwa wamelala ilipofika majira ya saa saba usiku Mayala alitoka nje kwa lengo la kujisaidia.

Alifafanua akiwa nje ghafla aliona kundi la watu wakiwa na mapanga na marungu huku wakimulika Tochi pande zote za nyumba yake ambapo alisikia sauti zikimwamuru atoke nje hali iliyomlazimu kuondoka katika eneo la nyumba yake huku akijiburuza kwa kutumia magoti.

Aidha Mayala alisema akiwa pembeni mwa mji wake aliona moto ukiwaka kwenye nyumba yake huku tochi zikimulikwa kila kona ya nyumba yake huku wakirusha mawe.

Hata hivyo mzee huyo alidai siku za nyuma lilifika kundi la watu watano nyumbani kwake ambapo walimwambia yeye ndiye amekuwa akizuia mvua kutonyesha na kumwamuru aondoke katika kijiji hicho.
‘Ndugu zangu waandishi wa habari watu wamepania kuniua kwani hii ni mara ya pili mwezi uliopita walikuja watu watano nyumbani kwangu wakinituhumu mimi nazuia mvua kutonyesha na nilipowakatalia walinipiga fimbo mkono wa kushoto ambao bado nauguza jeraha” alisema Mayala.

Mke wa Mayala alisema akiwa nyumbani kwake Aprili 12 majira ya saa saba usiku alisikia kundi la watu likiwa nje likimwamuru mme wake atoke nje ambapo aliwajibu kuwa mumewe hayupo.

Kutokana na hali hiyo kundi hilo lilivunja mlango na kumtoa mama huyo nje huku wakimfunika nguo machoni  na wengine wakichoma nyumba yake.

Aliongeza kuwa baada ya kuchoma nyumba walianza kumshambulia kwa bakora ili aweze kuonyesha mume wake alipo hata hivyo mama huyo aligoma na ndipo waliamua kuondoka

Kwa upande wake Mwenyekiti wa serikali ya kijiji cha Mwakwangu Matogolo Lushegembe amekiri kuvamiwa kwa wanandoa hao wawili ambapo ameahidi kuitisha mkutano wa hadhara ili kuweza kujadili suala hilo.

Kwa upande wake kamanda wa polisi mkoa wa Tabora Suzana Kaganda hakuweza kupatikana ili kuweza kulizungumzia suala hili hata alipopigiwa simu yake iliita pasipo kupokelewa.

No comments:

Post a Comment