Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Tuesday, 14 April 2015

TASAF WAAGIZWA KUWATUMIA WAANDISHI WA HABARI



Na Hastin Liumba, KigomaWARATIBU wa miradi ya TASAF ngazi ya mkoa na wilaya wametakiwa kushirikiana na vyombo vya habari ili kuelimisha jamii lengo na umuhimu wa mpango wa TASAF awamu ya tatu.



Hayo yamebainishwa katika kikao kazi cha Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) kikihusisha waandishi wa habari zaidi ya 70 kutoka mikoa ya Tabora, Rukwa, Katavi na Kigoma, waratibu wa TASAF, wahasibu na wasimamizi wa miradi hiyo toka wilaya zote za mikoa hiyo kilichofanyika Kigoma.

Mkurugenzi wa TASAF anayeshughulika Uwezeshaji Misheli Fariji akiwasilisha mada ya Ushiriki wa Vyombo vya Habari katika Kuelimisha Umma juu ya lengo la mpango huo wa kunusuru kaya maskini, alisema waratibu na wasimamizi wa mradi huo wanapaswa kutoa taarifa kwa waandishi wa habari ili zitangazwe kwa wananchi kwa kuwa kila mtu anayo haki na uhuru wa kupata habari pasipo kuathiri sheria za nchi kwa mujibu wa katiba ya mwaka 1977 ibara ya18.

'Ili kurahisisha utoaji elimu kwa jamii tutashirikiana na waandishi wa habari wa vyombo vyote kuelimisha jamii nchini kote, na naagiza Waratibu wote wa TASAF katika ngazi za mikoa na wilaya... wapeni ushirikiano mkubwa ili waandike habari zenu, wekeni bajeti ya kuwawezesha ili watusaidie kazi hiyo', alibainisha.

Aidha aliongeza kila raia ana haki ya kupewa habari wakati wowote inayohusu matukio au mipango mbalimbali inayohusu jamii pasipokuathiri sheria za nchi, hivyo akawataka waandishi wa habari kuandika habari nyingi zitakazo saidia jamii kuelewa lengo na umuhimu wa mpango huo unaotekelezwa na TASAF awamu ya tatu .

Naye Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa habari mkoa wa Kigoma Deogratius Nsokolo akiwasilisha mada juu ya Maadili ya Uandishi wa Habari katika kikao kazi hicho aliasa waandishi wa habari kuandika habari zitakazo saidia kuelimisha jamii.

Alisema kalamu za waandishi wa habari ni muhimu katika jamii kwani hufikisha ujumbe husika kwa wepesi zaidi, hivyo ni vema waandishi wakafuata maadili ya kazi zao ili kufikisha ujumbe kwa jamii.

Akichangia mada hiyo Mwandishi wa gazeti la Tanzania Daima mkoani hapa Emmanuel Seni alisema waandishi wa habari wanaoandika habari zisizofuata maadili wanaweza kuipotosha jamii lakini pia wanahatarisha usalama wao wenyewe hivyo akashauri kila mwaandishi kuzingatia maadili ya taaluma yake.

Mtaalamu wa Habari na Mawasiliano wa TASAF Zuhura Mdungi alivitaka vyombo vyote vya habari kutekeleza wajibu wao ipasavyo kwa kutoa elimu sahihi kwa jamii ili kufanikisha malengo ya mpango huo wa kipekee uliodhamiria kuinua kaya maskini kiuchumi huku.

‘Naahidi kuendeleza ushirikiano kwa vyombo vyote vya habari, na naomba waratibu wote  wa wilaya na mikoa muwape ushirikiano waandishi wa habari pasipo ubaguzi ili waandike kwa wingi habari zinazohusiana na mpango huo wa kunusuru kaya maskini," alimalizia.

No comments:

Post a Comment