NA MATUKIODAIMABLOG
MKUU wa mkoa wa Njombe Dr Rehema Nchimbi amempongeza mbunge Ludewa mkoani Njombe Bw Deo Filikunjombe kwa kutumia sikukuu ya pasaka kuwaandalia chakula watu wenye matatizo wakiwemo wafungwa wa gereza la Ludewa na wagonjwa waliolazwa katika Hospitali ya wilaya ya Ludewa huku akiagiza Halmashauri ya Ludewa kuanzisha huduma ya chakula kwa wagonjwa .
Dr Nchimbi alitoa pongezi hizo jana wakati alipoungana na mbunge huyo na viongozi mbali mbali wa mkoa na wilaya ya Ludewa kushiriki hadla hiyo ya mbunge kula chakula pamoja na wagonjwa na kuwapa misaada mbali mbali kama ulivyoutaratibu wake kwa kila sikukuu kula na wagonjwa na wafungwa .
Alisema utaratibu unaotumiwa na mbunge huyo ni utaratibu mzuri ambao unapaswa kuigwa na wabunge wengine nchini kwa kuyatembelea makundi mbali mbali ya kijamii wakati wa sikukuu ama siku nyingine badala ya kusherekea sikukuu kwa kufanya anasa.
'kweli ni jambo la kumpongeza sana mbunge Filikunjombe kwa huu utaratibu ambao amekuwa akiufanya binafasi niliposikia mbunge anakuja kufanya jambo hili kubwa la kula na wagonjwa pasaka niliamua kufunga safari na mimi kuja kushiriki zoezi hili na kumtia moyo zaidi mbunge kwa hili si wabunge wote ambao wanakawaida ya kutembelea na kuwafariji wagonjwa na wafungwa kama hivi 'alisema mkuu huyo
Hata hivyo mkuu huyo wa mkoa alisema kuwa katika kumuunga mkono mbunge Filikunjombe kwa wazo hilo zuri kwa upande wake anachangia ngunia 5 za mahindi ili kuwaanzishia wagonjwa wanaofika kujifungua huduma ya chakula kwa kipindi chote wawapo hospitalini hapo kama njia ya kuepusha wagonjwa kuwa na mawazo ya wapi watapata chakula
kwani alisema si wagonjwa wote wanaofika kusubiri muda wa kujifungua hospitalini hapo wanauwezo wa kiuchumi hivyo kuiagiza halmashauri ya wilaya ya Ludewa kuangalia uwezekano wa kuchangisha chakula kwa wananchi ili kusaidia huduma ya chakula kwa wagonjwa .
Alisema wilaya ya Ludewa na mkoa wa Njombe kwa ujumla hauna shida ya chakula kama ilivyomikoa mingine hivyo uwezekano wa kuanzisha utaratibu wa kutoa chakula kwa wagonjwa unawezekana .
Akishukuru kwa msaada huo wa chakula kwa niaba ya wagonjwa wengne waliolazwa hospitalini hapo paroko wa kanisa la anglikana ludewa Andrew Hiluka alisema kuwa alichokifanya mbunge huyo ni moja kati ya baraka kubwa kwake na kuwa baadhi ya wanasiasa wanapoteza nafasi zao kutokana na kuwa na roho mbaya na uchoyo kwa wale waliowachagua.
Kwani alisema Ludewa imepata kuwa na wabunge zaidi ya watano ila wakati wa sikukuu kama hizo wabunge hao walikuwa wakitoka nje ya Ludewa ama kujifungia na familia zao kula sikukuu tofauti na Filikunjombe ambae amekuwa ni mbunge wa aina yake kwa siku ya sikukuu kuandaa chakula cha pamoja na wagonjwa kwa kula nao chakula wodini .
Paroko Hiluka alitoa wito kwa wananchi wa jimbo la Ludewa kuendelea kumchangua kwa miaka mingine zaidi mbunge Filikunjombe kwani ametambua mahitaji sahihi ya wana Ludewa kwa kusaidia maendeleo ya jimbo hilo pia kuwagusa wote wenye matatizo mbali mbali ambao ni nje ya ahadi zake za ubunge .
Alisema ni kipindi cha Filikunjombe kasi kubwa ya maendeleo imeonekana kwa kila mwananchi wa wilaya hiyo na nje ya wilaya lakini pia ni mbunge pekee kusomesha sekondari watoto yatima zaidi ya 700 katika wilaya hiyo kwa kila mwaka huku wabunge waliopita labda aliyejitiahidi kusomesha basi haikuzidi watoto 2 kwa miaka yote mitano .
Nae mbunge Filikunjombe alisema kuwa utaratibu huo wa kula chakula na wagonjwa amekuwa akiufanya kila mwaka toka alipoingia madarakani mwaka 2010 na kuwa iwapo wananchi wa jimbo hili watamchagua ataendelea kuwaletea maendeleo lakini pia kuwasaidia watu wenye matatizo kwani anachoamini na kuendelea kuamini kuwa wazima na wagonjwa wote ni wapiga kura wake na kuwa furaha yake ni kuona wagonjwa wanapona ili waweze kumchagua tena.
CREDIT: MATUKIODAIMA.COM
|
No comments:
Post a Comment